Sunday, August 19, 2012

RVP akaribishwa katika mgahawa wa Rio Ferdinand (Rosso) kupata Dinner kusheherekea kujiunga na Man United

Robin van Persie na mkewe Bouchra wakiwasili Rosso Restaurant

ROBIN van Persie aliwasili jana jijini Manchester na usiku wa kwanza aliutumia katika mgahawa wa mchezaji mwenza Rio Ferdinand.


Mshambuliaji huyo, ambaye alizua gumzo kwa kukataa kuongeza mkataba Arsenal na kutimkia Manchester United wiki hii, alionekana akiwasili kwa chakula cha jioni katika mgahawa wa Rio uitwao Rosso.

Robin, 29 aliyeichezea klabu hiyo ya London kwa miaka nane kabla ya uhamisho huo wa kushangaza, aliwasili kwa chakula cha jioni akiwa amevalia Sweater-shirt nyeusi iliyoandikwa Mickey Mouse, na jeans iliyopauka huku akiwa ametinga viatu vya kufanyia mazoezi mepesi(simpo).

Alikua ameongozana  na mkewe na mama wa watoto wake wawili aitwaye Bouchra.
Bouchra mwenye umri wa miaka 28 alitinga skinny jeans iliyompendeza, top nyeusi yenye kola ya V, na jacketi jepesi la desaigner taupe suede kumachi rangi na viatu virefu (peep-toe heels).

       

Mgahawa wa kifahari wa Rio Ferdinand uliopo Manchester, uliopewa jina la kiitaliano ‘Rosso’ likimaanisha ‘Red’ kwa kiingereza ndipo alipo dine van Persie na mkewe.
Mgahawa huo una unaoweza kuchukua watu 150 kwa wakati mmoja, pia una Bar kubwa ambapo mara kwa mara wachezaji na watu mashuhuri hupendelea kujivinjari baada ya kazi..

                                 

Badboy Mario akiingia na mpenzi wake, Wayne Rooney, Mikey Owen na Michael Carrick wakitoka kupata lunch ni kati ya watu maarufu ambao huenda katika mgahawa huo wa Rio Ferdinand, Rosso.


First night ... Robin van Persie akishuka kwenye gari kuelekea kupata dinner katika mgahawa wa Rio Ferdinand

No comments:

Post a Comment