Friday, August 24, 2012

David Silva Agoma Kurefusha Mkataba Mpaka Alipwe Sawa na Y. Toure


David Silva anaendelea kugomea kusaini urefushwaji wa mkataba wake na Manchester City mpaka ombi lake la kupewa pauni 200,000 kwa wiki sawa na Yaya Toure pamoja na Vicent Company likubaliwe.

David Silva happy to let Manchester City sweat in his quest to gain parity with club's £200,000-a-week top earners


City na Wawakilishi wa Silva bado hawajafikia makubaliano kuhusu mkataba huo mpya, ingawa mikutano baina ya pande hizo mbili yamekuwa yakifanyika tokea mwezi Juni.

Vizito wa City wanasisitiza hawana wasiwasi juu ya suala la Silva kurefusha mkataba na bado wana matumaini  ya kufikiwa makubaliano na Mspanishi huyo kurefusha muda wake wa kuwepo klabuni.

Ila, mapatano yanaonekana yataendelea ndani ya msimu huu kutokana na kushindwa kuafikiana na Silva mapema, tokea alipojiunga June 2010 akitokea Valencia amefanya vizuri sana hilo ndilo linalompa jeuri ya kuamua alipwe kiwango gani.

Akiongea baada ya ushiriki wake katika mashindano ya Ulaya 2012, Silva alisema: " Maajenti wangu wanakaribia kufikia makubaliano na City na inaonekana tutafunga dili muda mfupi kuanzia sasa."

The playmaker dazzled last season for Manchester City and helped Spain to the European Championship trophy this summer
Silva: anataka alipwa angalau sawa na Teves 

Alisaini mshahara wa pauni 130,000 kwa wiki alipojiunga akitokea Valencia, ila baada ya kuibuka na kuwa muhimu katika kikosi cha Mancini, Silva na wawakilishi wake wanaona kuna kila sababu ya kulipwa sawa na kina Yaya Toure na Vicent Kompany.

City walisitisha kupatana na mchezaji mwingine Nigel de Jong majira ya joto yaliyopita kutokana na kile walichokiona kuwa mapendekezo makubwa ya mshahara, ila kwa inavyoonekana mapatano na Silva hayatositishwa bali yataendelea kutokana na umuhimu wake kwenye timu.

Silva, ambaye alikiri kupata shida kuzoea mafundisho ya Mancini alipofika, yuko wazi juu ya kujifunga katika mkataba mrefu na City, ingawa vyanzo vya Uhispania vinadai Barcelona wanamuona kama ndiye mrithi wa mchezeshaji Xavi.

City wana sera ya kutokufanya mazungumzo ya mikataba na wachezaji katikati ya msimu.

Mkataba wa Silva utafikia kikomo Juni 2014, hivyo City bado wanamuda wa wa kutosha kuendelea na mazungumzo kwa kujidai mpaka wanakapofikia makubaliano.

 

Wachezaji wa City Wanaolipwa Zaidi

       - Yaya Toure: pauni 200,000 kwa wiki

       - Vicent Kompany: 200,000 kwa wiki

       - Carlos Tevez: 198,000 kwa wiki

       - Sergio Aguero: 190,000 kwa wiki

       - Emmanuel Adebayor: 175,000 kwa wiki (Ametimkia Spurs)

USIKU MWEMA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!1

No comments:

Post a Comment