Wednesday, August 22, 2012

Welbeck Akubali Kuongeza Mkataba Man United


Mchezaji chipukizi wa Uingereza Danny Welbeck mwishowe amekubali kuendelea kuwepo Old Trafford mpaka 2016 - amekuwepo hapo tokea akiwa na miaka 8.

Life's a bench: Danny Welbeck goes off, Robin van Persie comes on against Everton... still, he didn't do much

Welbeck amekubali kupigania namba yake licha ya kuwepo ushindani mkubwa                               

Mshambuliaji huyo wa Manchester United amesaini mkataba mpya wa miaka minne ambao utamfanya aendelee kuwepo klabuni hapo mpaka mwaka 2016.

Kwa mara ya kwanza mchezaji huyo alicheza mechi yake ya kwanza mwaka 2008 ila katika miezi 18 iliyopita amejikuta akiwa miongoni mwa wachezaji muhimu wa kikosi cha kwanza.

Alianza kucheza timu ya wakubwa mwezi March 2011 na kufanikiwa kuchaguliwa na timu yake ya Taifa kwenda kwenye mashindano ya Euro.

Ingawa United wamemsajili Robin kwa kitita cha pauni milioni 24 mapema mwezi huu hapakuwa na shaka Welbeck angekubali kusaini mkataba mpya.

One Lion: Welbeck's England career has taken off - here he is having a pop against Italy in the Polkraine

Welbeck akitupiamo dhidi ya Italyalipoiwakilisha Uingereza mashindano ya Euro 2012

"Danny amekuwa hapa tokea akiwa na miaka nane na amebadilika sana katika miaka ya hivi karibuni - kwanza akienda kwa mkopa na mwaka jana kama mchezaji wa kikosi cha kwanza," Sir Ferguson alinena kwenye mtandao wa manutd.com.

"Amekuwa mchezaji muhimu timu ya taifa pia, na kaonesha ukomavu wa utendaji wake Euro 2012.

"Mwaka huu utakuwa muhimu kwake, kuna matarajio makubwa juu yake."

Beck and haul: Danny Welbeck got among the goals for United last season, including here against Arsenal

Danny Welbeck hujituma na pia hufunga: hapa akiwa amefunga moja ya magoli dhidi ya Arsenal 

Welbeck, aliyezaliwa Longsight, alionesha furaha yake baada ya kusaini mkataba mpya na klabu yake tokea akiwa mvulana.

"Kuchchezea United ndio hasa nilichokua nataka kufanya - ni klabu niliyoisapoti maisha yangu yote," alisema.

"Nina hamu sana na msimu mpya ili nitoe mchango wangu kusaidia timu kushindania mataji.

"Nina jifunza kila mara kutoka kwa meneja bora na nina shauku hili liendelee nikiwa na wachezaji wakiwango cha dunia kikosini."

Welbeck amefunga jula ya magoli 17 ndani ya michezo 64 akiwa United tokea alipocheza mechi yake ya kwanza dhidi ya Midlesbrough katika kombe la ligi Septemba 2008.

PONGEZI KWA WELBECK KWA KUAFIKIANA NA MAN U, CHERIOOOO!!!!!!!!!!

No comments:

Post a Comment