Friday, August 24, 2012

Sahin Abadili Mawazo Sasa Aitaka Liverpool Badala Ya Arsenal


Hivi leo pametokea kutokuelewana kati ya Arsenal, Real Madrid na mwakilishi wa Sahin kuhusu makubaliano ya uhamisho wa kiungo huyo. 

Madrid wanataka wamtoe kwa mkopo kisha mwisho wa mkopo huo yafanyike mazungumzo juu ya kuchukuliwa jumla ama kuhitajika kurudi Bernabeu kitu ambacho hata Sahin ndicho anachoafiki, Arsenal wao hawataki habari za mkopo zaidi ya kutaka kumnunua jumla.

On the move: Nuri Sahin of Real Madrid

Nuri Sahin

Real walitoa saa 24 ili Arsenal kubadili msimamo wao, ila mpaka masaa hayo yanaishia upande wa kambi ya Arsenal ulikua kimya.

Mwakilishi wa Sahin alisafiri leo Alhamisi asubuhi kwenda Liverpool kukamilisha taratibu za Sahin kujiunga na timu hiyo, baada ya kuchoshwa na longolongo za Wapiga Bunduki Wa London. 

Kama FullSoka ilivyoripoti kwenye kurasa yake ya facebook (www.facebook.com/fullsoka) kukubali kwa Sahin kujiunga na Arsenal mwanzo wa wiki hii, baada ya kuwaambia Real kuwa Emirates ndio mahali alipochagua kwenda kwa mkopo.

Ila katika mazungumzo na mwakilishi wake Reza Fazeli, ilijitokeza kwamba Arsenal hawakutaka makubaliano ya mkopo badala yake kufanya manunuzi ya jumla kwa haraka.

Real hawakuwa radhi kwa hilo, kama ilivyokuwa kwa sahin, ambaye alikua anataka aende Arsenal kwa miezi 12 ili ajue kama Real watakua bado wanamuhitaji kabla hajaamua kujikita kwenye masuala ya kuihama jumla.

The Arsenal groundsman marks out the Emirates Stadium pitch

Emirates Stadium: hapa hasa ndipo Nuri Sahin anapotaka kuwepo kwa mkopo

Kwa upande wa Liverpool wanaafikiana na Real pamoja na matakwa ya Sahin, na ndio sababu jioni hii ajenti Fazeli yupo Merseyside kuweka wazi makubaliano na MD wa Liverpool Ian Ayre.

Mpaka sasa bado usajili haujakamilika na Arsenal wana nafasi bado, ingawa Real wanaamini kiungo huyo atakwenda Anfield, baada ya kuweka wazi wangependa aende huko.

Mapema leo, gazeti moja la Uhispania liliripoti kwamba hatma ya Sahin itajulikana ndani ya siku moja ijayo. 

Liverpool ndio ilikua timu ya kwanza kuonesha nia ya kumchukua, ila Sahin alipendelea zaidi kwenda Arsenal na alitaraji mpaka Jumanne iliyopita kua angekuwa ametimiza ndoto yake ya kucheza chini ya bosi wa Arsenal Arsene Wenger.

Gazeti la Macca waliandika kwamba Liverpool walitaraji kuwa wamekamilisha usajili huo wa mkopo kufikia leo Alhamisi jioni, ingawa gazeti la Mirror linaona suala bado ni tete kukamilishwa haraka kiasi hicho.

Gazeti lingine la Madrid liliandika kwamba Liverpool imejitokeza kua timu inayomfaa zaidi Sahin, kwani Sahin mwenyewe ana uhakika kwamba maneja wa Liverpool Brendan Rodgers atamuhakikishia nafasi kwenye kikosi kinachoanza kulinganishwa na Arsenal walio na viungo wengi.

USIKU MWEMA!!!!!!!!!!!!!!!

No comments:

Post a Comment