Thursday, August 23, 2012

Man U Kuuza Watatu Kabla Ya Dirisha la Usajili KufungwaBaada ya Mashetani Wekundu kufanya usajili unaoonekana kushiba, Sir Ferguson ana kazi pevu kuhakikisha baadhi ya wachezaji walio nje ya kikosi cha kwanza wanaotarajia kucheza kuwatoa kwa mkopo ama kuuza jumla.

Wachezaji kama Dimitar Berbatov, Federico Macheda na Bebe wanaonekana kutokua na nafasi hata la kukaa benchi hivyo wanaotakiwa kutafuta pori kuanzia sasa mpaka tarehe 31 (siku ya mwisho ya dirisha la usajili).

Pia imeripotiwa watu wa juu Old Trafford, wamesisitiza kua Nani na Hernandez hawataruhusiwa kuondoka Manchester.

Berbatov ana hamu ya kuondoka Man U, ila si kwa Bebe na Macheda ambao wangependa kubakia.

Dimitar Berbatov
Berbatov: Hana anachotamani zaidi ya kuondoka 
M-Bulgaria huyo ana uhakika wa kutakiwa na timu nyingi licha ya kua na umri wa miaka 31 baada ya kuchoshwa na benchi la Old Trafford.

Ferguson anaonekana kua mgumu kumuuza mchezaji huyo wa zamani wa Spurs kwa bei "chee" ila bado haijajulikana hasa Mzee huyo anataka kiasi gani.

Kuna hatari ya kuondoka bure msimu ujao iwapo hatoruhusiwa kusajili timu nyingine majira haya.

Ni vigumu kukisia timu gani zitahitaji huduma za Bebe na Macheda, kwa kuwa ni washambuliaji ambao kwa timu yoyote kuwachukua basi itakua ni kubahatisha.

Mreno Bebe ni maarufu sana! si kwa kucheza mpira bali kwa kununuliwa kwa kitita cha pauni milioni 7.4 bila hata Mzee Ferguson kuwa amemuona akicheza mpira.

Akiwa na miaka 22 sasa, msimu uliopita alikua kwa mkopo Besiktas ila maumivu ya kano (ligament) yalimfanya awe nje ya kiwanja kwa takribani miezi sita. Amerudi Premier League ila haonekani kuwa na future Old Trafford kwa kushindwa kwake kuthibitisha thamani yake.


Macheda: Nafasi ni finyu hata ya kukaa benchi  
Kwa upande wa Federico Macheda alionesha kua ni muona nyavu wa hali ya juu alipopewa nafasi kwa mara ya kwanza, akifunga goli muhimu na la ushindi dhidi ya Aston Villa muda wa majeruhi.
Hata hivyo Muitaliano huyo hajawahi fikia tena kiwango hicho na kupelekwa kwa mkopo Sampdoria na QPR havikusaidia kuchochea kurudi tena kwa kiwango chake.
Ferguson hatokuwa na nafasi ya wachezaji hao watatu msimu huu ukizingatia kuwepo kwa Wayne Rooney, Robin Van Persie, Chicharito na Danny Welbeck.
MCHANA MWEMA WA ALHAMIS!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

No comments:

Post a Comment