Sunday, August 19, 2012

Man City kumuongezea mkataba mnono Balotelli


Mabingwa wa  Premier League wana wasiwasi thamani ya Balotelli itapungua hivyo wanapanga kukaa nae mezani ili kumshawishi kusaini mkataba mrefu zaidi na wenye maslahi bora.

Mario Balotelli - Manchester City
 Balotelli atazawadiwa mkataba mnono kutokana na timu nyingi kuanza kumuwinda.
Straika huyo mwenye vituko, mkataba wake wa sasa utamalizika 2015 ila City wanataka waongee nae mapema kuhusu kuurefusha mkataba wake kabla ya Mwaka Mpya.

Mabingwa hao wa Premier League walikataa pauni milioni 40 kutoka kwa matajiri Paris-Saint Germain majira haya ya usajili na kujitahidi kuzuia maombi mengi ya timu za Serie A.

Miaka miwili ya Balotelli Etihad Stadium imekua ni ya utata ndani na nje ya kiwanja, huku bosi Roberto Mancini akionesha dhahiri kukasirishwa na na matendo ya muitaliano mwenzake huyo.

Lakini hayo yote sio tija kwani wasiwasi umewatanda na wanajitahidi kutokuruhusu miaka iyoyome kufikia miwili ya mwisho kitu kitakachosababisha thamani yake ya mauzo kuanza kupungua.
Je Balotellit atawatunishia misuli Man City kumpa mshahara anaoutaka. 
Goal.com  imeripoti kwamba klabu hiyo ya Manchester ipo tayari kumfanya mchezaji huyo aliyetimiza miaka 22 wiki iliyopita kuwa kati ya wachezaji anaolipwa vizuri duniani.

Balotelli sasa anachukua mshahara wa pauni 110,000 kwa wiki na mazungumzo yatalenga kumfanya alipwe kama wenzake kina David Silva, Sergio Aguero na Carlos Tevez ambao hulipwa pauni 200,000 kwa wiki kila mmoja.

Mshambulizi huyo anawakilishwa na ajenti maarufu Mino Raiola, ambaye hivi karibuni alidai kwamba Balotelli ana thamani ya pauni milioni 200 kufuatia mchezo mzuri aliyouonesha kwenye mashindano ya Euro 2012.

Ajenti huyo ndiye aliyewezesha Zlatan Ibrahimovic's kuuzwa na AC Milan kwa pauni milioni 29 kwenda PSG, na kumfanya awe analipwa mshahara wa pauni 250,000 baada ya kukatwa kodi.

Balotelli husisitiza ana furaha kuwa Manchester ila hua hakatai kama siku moja anaweza rudi nyumbani Italy ama kwenda kuchezea timu kubwa mojawapo ya Uhispania (Barca, Real) katika miaka ijayo.  

No comments:

Post a Comment