Friday, August 24, 2012

Nani Aondoa Ombi la Kuongezewa Mshahara Ili Abakie Man U


Nani ameondoa ombi lake la kutaka kuongezewa mshahara ili kuingia mkataba mpya Old Trafford. Mreno huyo na washauri wake wako tayari kukubali mshahara wa awali (basic Wage) uendelee kuwa ule ule anaopewa sasa ila awe bonus ndio ziongezwe.Hali ya nani kuendelea kuwepo Old Trafford inatia mashaka. Ameondolewa kwenye kikosi cha mechi ya kesho dhidi ya Fulham baada ya mchezo usioridhisha Jumatatu dhidi ya  Everton katika uwanja wa Goodison Park. 


Ukichanganya na kiwango kibovu alichoonesha mwishoni mwa msimu uliomalizika, imekua ndio sababu ya msingi ya matakwa yake ya mkataba mpya kutupiliwa mbali na United.

Nani
Nani: Mambo magumu sasa ataka pungufu

No comments:

Post a Comment