Wednesday, August 22, 2012

Emmanuel Adebayor Auzwa Bei Ya Kutupa na Man City

                                                               
Sorted: The long-running Emmanuel Adebayor transfer story is done
Ade Mabao: Atalipwa mshahara wa pauni 175,000 kwa wiki. 

Emmanuel Adebayor amekamilisha mipango ya kuhamia Tottenham Hotspur kutoka Machester City kwa bei ya kutupa pauni milioni 5 tu.

Alifanya vizuri msimu uliopita , akichezea Tottenham kwa mkopo, alifunga jumla ya magoli 17 katika ligi kuu ya Premier.
Adebayor atakua mmoja kati ya wachezaji wa Spurs wanaolipwa mshahara mkubwa. 
Adebayor mwenye miaka 28, alikuwa akilipwa na Manchester City pauni 175,000 kwa wiki.
Mshambulizi huyo wa zamani wa Arsenal, alivujisha habari hizo kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter akiandika: Tottenham niko njiani! natamani magoli. Kaeeni tayari.
Mkataba wa Adebayor ulibakisha miaka miwili zaidi kama mchezaji wa Man City, ila tokea kuwe na kutokuelewana na Mancini amekua akipelekwa kwa mkopo kwenye timu kadhaa: (Real Madrid na Tottenham).
 " Nafurahi kujiunga moja kwa moja na Spurs baada ya klabu kuelewana na manchester City, alisema Adebayor.".
Tottenham na Man City hatimaye wafanya mapatano juu ya mshahara wa Adebayor wa pauni 175,000 kwa wiki 


"Pengine ilichukua muda mrefu kinyume na ilivyotarajiwa, lakini nimefurahi sana kurudi Tottenham Hotspurs. Nilifurahia sana nilipokua hapa msimu uliopita, na ni matumaini yangu tutaweza kwa pamoja kufanikiwa zaidi."
Inafahamika kwamba Spurs waligoma kumpa Adebayor mshahara wa pauni 175,000 kwa wiki.
Naye Adebayor aligoma akitaka apewe pauni 175,000 ama arudi City kukaa benchi kusubiria mkataba wake na City uishe huku akiendelea kulipwa kiwango hicho hicho. 
Mkataba wake kuisha maana yake atakua huru na pesa yote ya uhamisho atapokua anasajili timu nyingine itakuwa ya kwake.
Kwa kua Adebayor kurudi City atakuwa hatumiki huku akiendelea kulipwa pauni 175,000 kwa wiki kwa kipindi cha miaka miwili ijayo, City wakawa hawana jinsi ila wakubali kulipa zaidi ya nusu iliyobaki kujalizia mshahara kufikia pauni 175,000, na pesa hiyo ya kufidia ikitoka kwenye ada halisi ya uhamisho hivyo mwishowe City wakaambulia pauni milioni 5. 
Tottenham watamlipa pauni 80,000 kwa wiki, na Man City kufidia pauni 95,000 kwa kila wiki, ili kufanikisha makubaliano kati ya vilabu hivyo viwili.

JUMATANO NJEMA!!!!!!!!!!!!.

No comments:

Post a Comment