Tuesday, August 28, 2012

Nani Anakaribia Kuhamia Zenit kwa Pauni Milioni 25


Timu ya Zenit St. Petersburg wanatarajia kuwasilisha ofa ya pauni milioni 25 kwa ajili ya winga wa Manchester United Nani, ambaye mpaka sasa hawajakubaliana na United kuhusu mkataba mpya.

Imeripotiwa kwamba wawakilishi wa Louis Nani wamekutana na timu ya Zenit kwenye jiji la Amsterdam jana Jumatatu jioni kuongelea uwezekano wa uhamisho huo.

Wanted: Manchester United midfielder Nani (left) could be heading for Russia
Louis Nani katika mechi aliyovurunda dhidi ya Everton
"Habari kuhusu Nani ni kweli, tunamtaka' Kocha wa Zenit Luciano Spallettu alithibitisha mapema mwezi huu.
'Ila itategemea na kiasi gani United watataka tuwalipe kwa sababu hatuwezi kulipa zaidi ya bei tunayodhani ndiyo thamani yake halisi.'

Nani Trademark: Tutamisi mambo yake iwapo ataondoka
Alipoulizwa zaidi, alisema: " Siongelei ofa kwa ajili ya mchezaji fulani, naongelea ofa kwa klabu yake." Alimalizia kocha huyo.

Tottenham pia inasemekana wanamtolea macho ila ada ya pauni milioni 25 si rahisi wao kulipa.
Mbali na Nani, Anderson pia amepewa ovyo la mwisho kukaza buti kuwa fiti kama si hivyo atawekwa sokoni. 
JUMANNE NJEMA!!!!!!!!!!!!!!!

No comments:

Post a Comment