Sunday, August 19, 2012

Sahin achagua kujiunga na Arsenal


Kwa habari za uhakika zilizotolewa na gazeti mashuhuri la Uhispania Marca, Arsenal wako mbioni kukamilisha mkataba na Real Madrid ili kumsajili kiungo Mturuki Nuri Sahin kwa mkopo wa mwaka mmoja.
Kiungo huyo mwenye miaka 23 alisaini mkataba wa miaka sita Bernabeu majira ya joto ya msimu uliopita akinunuliwa kutokea Borussia Dortmund, kipindi chote hicho amepata wakati mgumu kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza, na hilo lilichangiwa sana kuumia akiwa hata msimu haujaanza.
Sahin hakutumiwa kwenye mechi za kirafiki za hivi karibuni za Real Madrid na anasadikiwa atawasili London hizi punde kukamilisha taratibu za usajili. 
Inaaminika kwamba timu hiyo kubwa  Uhispania walijaribu kumtumia Sahin kama chambo cha kumpata Luka Modric wa Spurs, ila lengo hilo liligonga mwamba kwani Sahin amekataa kwenda  White Hart Lane.
Kama Sahin atatia saini kwenye mkataba, basi  atakua mchezaji wa nne kwa Arsenal kusajiliwa majira haya ya joto.
EID MUBARAK!!!!!!!!!!!!!!!

No comments:

Post a Comment