Tuesday, July 3, 2012

"MAANA YA "NAMBA 9 YA UONGO" "MABEKI WA UONGO", SPAIN NA BARCELONA

      KADRI miaka inavyokwenda mpira wa miguu unaobadilikabadilika . Mabeki kujishughulisha zaidi na mashambulizi kuliko kakaba hasa wa pembeni (Attack to Defend). Mawinga kucheza upande tofauti na miguu waliozoea kuitumia. Messi kucheza kulia huku akitumia zaidi mguu wa kushoto ili kuelemea ndani mwa kiwanja kupata fursa ya kufunga zaidi kuliko kupiga krosi.



Tukianza na "Namba 9 ya Uongo" ( False No 9), ni mchezaji kupangwa kama muongoza mashambulizi ilhali hakai kabisa kwenye eneo tunalotarajia namba tisa apatikane ila anarudi nyuma kabisa kurandaranda akitafuta mpira. 
Kwa maneno mengine ni kinyume na mshambuliaji mviziaji (Poacher). 


Mfano ni Messi, fomesheni 4-3-3 ya Barcelona humfaa kufikia kufunga magoli zaidi ya 50 kwa msimu.


Pele, Maradona, Romario, Ronaldo De Lima hawa wote walicheza namba tisa tuliyoizoea kufunga magoli. Kwa kipindi kile isingeingia akilini kutegemea winga kufunga hata magoli kumi kwa msimu bila kucheza ndani ya kumi na nane.


Messi hupatikana nafasi ya winga tena nyuma kidogohuku akiwa ndio kinara wa mashambulizi. Ni muhali kumkuta kwenye box.


Mabeki: kiungo wa kati kucheza nafasi ya beki wa kati ( Mascherano wa Barca) ama Hummel wa Dortmund, ama beki wa kati kua na jukumu la kugawa mipira akicheza kama kiungo aliye mbele ya kipa wake kama achezavyo Gerard Pique wa Barcelona.


Hummel: Beki  mwenye majukumu kama ya kiungo B. Dortmund


Kitu muhimu kua beki wa aina hii ni ufundi wa kupiga pasi ndefu kwa usahihi. 
Hii ni kutokana na hatari iliyopo iwapo pasi aliyokusudia itakosewa, uwezekano wa kosa hilo kuleta madhara ya kuzaa goli ni mkubwa.


Vyuo vya soka vya kisasa vinatilia mkazo kwenye ufundi zaidi bila kubagua mabeki wa kati.
Matt Hummels wa Dortumund ni mhitimu wa akademi ya Dortmund inayosisitiza umiliki wa mpira na pasi, Phil Jones na Chris Smalling kwa kiwango kikubwa wamepata somo hilo pia. 


Viungo wamekua bora zaidi na majukumu yameongezeka, kukaba na kuchezesha timu ni jambo la kila kiungo wa kisasa. 


Javier Mascherano ama kama umeangalia mashindano ya UERO 2012 Daniele De Rossi, hawa hua mafundi wa kukaa na mpira kutoa pasi za uhakika ziada ikiwa ni wakabaji wazuri kitu kinachopelekea kutumika kama mabeki wa kati pale wanapohitajika. Wachezaji hawa ndio wanaotoa taswira ya "MABEKI UONGO"

Smalling na Jones: Ufundi  na maarifa zaidi ikibidi kwenda kufunga.  


Barcelona na Spain husisitiza:


" Usipoteze mpira, hakuna kuokoa mpira kwa kubutua bali kwa kutoa pasi kwa mwenzio, inapobidi kupiga mpira mrefu wa juu basi umfikie mwenzako. Kama hawafunguki endeleeni kupigiana pasi fupi fupi hata ikibidi mpira urudishwe nyuma kabisa, kumbuka usibutue bila malengo"


Kwa aina ya uchezaji wa Barcelona, wachezaji wote wanaokusanywa ukitoa kipa hua wamejaaliwa ufundi wa kutuliza mpira ( first touch) ukiwa kasi  na kujituliza na kutoa pasi katika mazingira magumu. 


Kama njia itakosekana hufundishwa kuwa watulivu na kuweka mpira katikati ya miguu yao mifupi  kusubiri nafasi ya kutoa pasi ama kupiga chenga ijitokeze, chaguo la mwisho kusubiri kufanyiwa madhambi pindi wapinzani watapolazimisha kupoka mpira. 


Kwa sababu hii wale mabeki wa kati tuliowazoea SITAKI MCHEZO hawana nafasi katika sistimu hii. Beki mwenye ufundi na utulivu wa hali ya juu ni yule ambaye hata kama kuna presha ataweza kuondoa mpira eneo la hatari bila kupiga mpira juu bila malengo.
Hapa tunawapata Mascherano kama kiungo na Pique kama KIUNGO ANAYECHEZA NAFASI YA BEKI WA KATI.



Pique na Mascharano mazoezini, kumiliki mpira ukiwa juu ama chini hupewa kipaumbele Barca.



Kwa kuanzia kiungo hadi kwa washambulizji wenyewe hufukuzia mpira kwa kasi ili kuogofya na kumzonga aliyeamua kuumiliki, nia ni kuwapresha wapinzani wacheze kwa kasi wanayoitaka.


Kasi hii itayopelekea wapinzani kupiga mpira bila malengo ama kutahamaki wamenyang'anywa wakiwa wanajaribu kufikiria cha kufanya. Mshambuliaji wa mwisho anategemewa kubadilishanabadilishana nafasi na vioungo, arudi nyuma kutafuta mipira na kukimbia haraka kwenye box pale mashambulizi yanapoanzishwa.


Sistimu hii ndio iliyodhihirisha Ibrahimovic hawafai, Barca ilibidi wabadili kidogo aina ya uchezaji kuendana nae na kwa kipindi hichi ndipo ilipogundulika kwamba  si Ibrahimovic aliyekua namba tisa ingawa yupo katika ineo la namba tisa bali mtu aliyekua pembeni Messi. Hapo ndio umuhimu wa namba tisa ukaanza kudhoofu.


Kwa majukumu ya namba tisa kuondolewa katikati na kupelekwa pembeni, ndipo dhana ya kina C. Ronaldo ama Messi kuchukuliwa kama ni NAMBA 9 WA UONGO.




Torres: Straika wa Spain aliyeongoza kwa magoli EURO 2012 ila anasubiri nje.
Spain chini ya Vicente del Bosque wanacheza system sawa na Barcelona, na humtumia David Villa kwenye position achezayo Messi Barca. Hata hivyo Villa akiwa majeruhi, Vicente del Bosque amewachagua Fabregas na Torres kwenye mashindano ya Euro. 


Fabregas ni mzuri kwenye kulinda mpira na kubadilishanabadilishana nafasi na viungo wengine, ila ana mapungufu linapokuja suala la umaliziaji. 


Kwa upande awa Torres ukiachilia maswahibu yaliyomkuta ni mfungaji hasa ila mpoteza mipira mzuri pia kitu ambacho ni kawaida kwa washambuliaji.


Suala la kupoteza mpira hua halina msamaha kwa Barcelona ama Spain, ndio maana Torres huanzia benchi na Ibrahimovic kufungasha virago.


Hili liko wazi na ni sababu washambuliaji waliokua moto wa kuotea mbali kwenye ligi ya EUROPA Llorente na Nagredo mpaka sasa hawajaichezea timu yao ya taifa Spain.



Ningependa kuona na wewe unachangia hapo...................................!!!!!


Kazi njema.

No comments:

Post a Comment