Tetesi huko Ulaya zinasema kwamba Manchester United wako mbioni kumnyakua Kaka kwa mkopo kabla ya dirisha la usajili kufungwa siku chache zijazo.
Gazeti la The Daily Mail, limeandika kwamba Bosi wa United Sir Alex Ferguson anafikiria kumsajili kiungo huyo wa Real Madrid kwa mkopo. Real Madrid inasemekana wanatafuta mnunuzi wa M-Brazili huyo kwani wana matumaini ya kumnasa  Luka Modric kutoka Tottenham Hotspur.
Manchester United imepewa ofa ya kumchukua Kaka kwa mkopo mrefu kwa kua Real Madrid wanajitayarisha kumpokea Luka Modric.
Galatasaray na timu ya zamani ya Kaka AC Milan pia wameonesha shauku la kumnasa mchezaji huyo Bora wa Dunia kwa mwaka 2007, lakini United ndio klabu inayomvutia M-Brazili huyo.
Mshahara wa Kaka ni karibia pauni 250,000 kwa wiki sawa na mishahara ya Van Persie na Wayne Rooney na ingawa Real wasingependa kumwachia Kaka ajiunge na wapinzani wao kwenye michuano ya Champions League, mshahara wake ni mzigo ikizingatiwa kwamba muda mwingi kwa msimu huu watatumia akiwa benchi Bernabeu.
Hi-res-137846443_crop_exact
Kaka: Hakuna kinachoonekana kumwendea vema Real
Akiwa katika kiwango cha juu kabisa cha uchezaji wake, mwaka 2009, Kaka alifanya uhamisho wa pauni milioni 60 kutoka AC Milan kwenda Real Madrid. Kwa uhamisho huo ulimfanya awe mchezaji mwenye thamani kubwa duniani kwa wakati huo.
Kwa nionavyo (FullSoka) mshahara wake ni mkubwa sana kwa Real Madrid kuendelea kua naye, na sidhani kama United wanaweza kuafiki kulipa mshahara huo—hasa sasa wakiwa na Wayne Rooney na Robin van Persie wakilipwa mshahara huo.
Hi-res-97616826_crop_exact
Hata waamuzi si wenye msaada kwake 
Usajili wa Alexander Buttner kutoka Vitesse Arnhem ni mfano mzuri wa usajili wanaoufanya Mashetani Wekundu kwa muda huu wa usajili uliobakia.
Wanahitaji beki wa kushoto kusaidiana na Patrice Evra, na inaaminika bado wanamfuatilia beki wa kushoto wa Everton Leighton Baines. Ingawa, Everton wanataka pauni milioni15 mpaka 17 kwa mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Uingereza. United hawako radhi kutoa kiasi hicho cha pesa, ndio maana wakamsajili chipukizi anayeinukia Alexander Buttner kwa pesa ndogo kuliko hizo.
Manchester United wanaonekana wana mzuka wa usajili, ila haionekani kama wanaweza kutoa mshahara wa pauni 250,000 kwa wiki zinazohitajika kumleta Kaka Old Trafford Kaka. Umri umeshakwenda, na si tena Kaka yule tunayemfahamu, isitoshe ana tatizo la kua majeruhi mara kwa mara, hata uchezaji wake umekuwa wa mashaka.
Pia sioni kwa nini Red Devils watamtaka mchezaji ambaye hana nafasi katika timu yake ya taifa (Brazil) au Real Madrid kwa kiwango hicho cha pesa.
Ila kuna wakati Sir Furguson hua hatabiriki na mwishoni uamuzi wake hulipa.........................haya na tusubiri.
JUMATATU NJEMA!!!!!!!!!!!!!!!