Saturday, August 25, 2012

Arsenal Kuuza Kiungo Mwingine AC Milan

Klabu ya Ac Milan kwa kinachoonekana mshangao kwa wengi wapo mbioni kumuhamisha kiungo mwingine wa Arsenal kujiunga na klabu hiyo ya San Siro, Sky Sports imedokeza.

Arsene Wenger Smile


Sky wanaendelea kudai kwamba kwa waonavyo wao Bosi wa Arsenal hatokuwa na pingamizi juu ya jambo hilo na ataruhusu kiungo huyo aondoke bila ugumu wowote.

Kocha wa Ac Milan Massimiliano Allegri yupo sokoni akitafuta kiungo mkabaji na Denilson ndiye hasa aliyeona anafaa.

Denilson kwa sasa yupo nchini kwao Brazil akiichezea klabu ya Sao Paulo kwa mkopo baada kushindwa kupata nafasi Arsenal.

Mbrazil huyo alianza kuchezea timu ya watoto ya Sao Paulo na kupanda ngazi zote za timu za vijana na mpaka kufikia kuwa nahodha wa timu yake ya Taifa Brazil(U-21) kabla Arsenal hawajamsajili August 2006.

Samba Boy: kuna uwezekano akaelekea San Siro 

Tofauti na alivyouzwa Alex Song na Robin van Persie kwenda Barca na United, ofa yoyote kuhusu Denilson itakuwa rahisi kwa Arsene Wenger kukubali kirahisi.

Kujua hasa kwa nini Ac Milan wamevutiwa naye ni vigumu kuelewa lakini labda Bosi huyo wa Rosseneri anajua nini anataka kutoka kwa kijana huyo wa miaka 24.

Kiungo Denilson alichukua muda kuzoea mfumo wa Arsenal ila alitokea kuwa mmoja kati ya wachezaji wa kikosi cha kwanza cha The Gunners mwaka 2008/09, akishiriki michezo 51. 

Baada ya hapo, kiwango duni alichokuwa akionesha katika miezi 18 iliyofuata ikawa sababu ya kupelekwa Brazil kwa mkopo.

Denilson: Alipojiunga na Sao Paulo kwa mkopo 

Na kuibuka kwa Jack Wilshare kulichangia kwa kiasi kikubwa kumuondoa na ikabidi atimkie Sao Paulo kwa mkopo kuokoa soka lake.

Wenger  amekua akijaribu kumuuza Denilson majira ya joto yaliyopita na iliposhindikana akamrudusha tena Sao Paulo kwa mkopo.

AC Milan inawezekana wanahisi kutokana na umri wa Denilson kuwa miaka 24 hivyo kuleta matumaini ya kufanya vizuri mbeleni. 

Kwa upande wa Arsenal ofa yoyote ya maana ni dhahiri itakubaliwa kwa kuwa si mchezaji anayeonekana kuwa kwenye mipango ya Arsene Wenger tena.

JUMAMOSI NJEEEEEEEEEEEEMA!!

No comments:

Post a Comment