Saturday, August 25, 2012

Ni Mataji 44 kwa Walioondoka Arsenal 0 kwa Waliobaki

Imepita miaka saba sasa tokea Arsenal walipotwaa kombe lao la mwisho la maana, na tokea wakati huo wachezaji waliyoihama klabu hiyo kujiunga na klabu zingine wamekusanya jumla ya medali za ushindi 44! 
Na si haba Song na van Persie hawatosubiri muda mrefu kabla hawajajipatia vikombe kupitia timu zao mpya.
Hapa FullSoka inaangalia ni vikombe vingapi wachezaji walioikacha Arsenal wameweza kupata ikiwa waliobaki hawajaambulia kitu. 

Tokea kulitwa kombe la FA mwaka 2005, Arsenal hawajaweza tena kutwaa kombe lolote kubwa na wameuza wachezaji wa kiwango cha juu 17 walioshinda jumla ya medali 44 kupitia timu 11 tofauti.
Samir Nasri akiwa na kombe la Premier League aliloshinda msimu 2011/12 
Thiery Henry, Cecs Fabregas, Samir Nasri, RVP na Song kwa kuorodhesha wachache waliihama Arsenal kwenda kutafuta makombe kama tukiamini maneno yao.

Arsenal imejikusanyia jumla ya pauni milioni 163 kwa mauzo ya walioondoka, bila kujumuiasha pauni 39 milioni za mauzo ya RVP na Song. 
Tunaposema mataji makubwa tunaondoa Community Shield na vikombe vya namna hivyo kwenye ligi zingine.
Debayor: Kombe lake la kwanza kubwa alilipatia Real 

Unaweza sema mmmh, si wamekwenda timu kubwa, lakini wengine wamepata vikombe na timu ambazo hata kwa sasa hazipo tena kwenye ramani ya Ligi Kuu: PORTHSMOUTH (FA Cup- medali kwa Sol Campbell na Lassana Diara) na BIRMINGHAM (Carling Cup - medali kwa Seb Larsson na Alex Hleb).                                   


Mataji Waliyopata Wachezaji Walioihama Arsenal Tokea 2005

2005 ---  PATRICK VIEIRA akiwa Juventus: 3 Serie A titles (Inter), 1 FA Cup (ManCity).

2006 ---  SOL CAMPBELL akiwa Portsmouth: 1 FA Cup. 

2006 ---  ASHLEY COLE akiwa Chelsea: 1 Prem Lge, 4 FA Cups, 1 Lge Cup, 1 Champs Lge. 


2006 ---  SEBASTIAN LARSSON akiwa Birmingham: 1 Carling Cup.

2006 ---  LAUREN akiwa Portsmouth: 1 FA Cup. 

2006 ---  JOSE ANTONIO REYES akiwa R Madrid: 1 La Liga, 1 Portuguese Lge Cup 

                (akiwa Benfica), 2 Europa Lge, 1 Uefa SuperCup 

2007 ---  THIERRY HENRY akiwa Barcelona: 2 La Liga, 1 Spanish Cup, 1 Champs Lge, 

                1 Uefa SuperCup, 1 Club World Cup. 

2007 ---  LASSANA DIARRA akwa Portsmouth: 1 FA Cup, 1 Spanish Cup (akiwa R  

                Madrid), 1 La Liga.

2008 ---  MATHIEU FLAMINI akiwa Milan: 1 Serie A. 

2008 ---  ALEXANDER HLEB akiwa Barcelona: 1Champs Lge, 1 La Liga, 1 Spanish 

                Cup, 1 Lge Cup (akiwa Birmingham).

2008 ---  GILBERTO SILVA akiwaa Panathinaikos: 1 Greek Lge, 1 Greek Cup.

2009 ---  EMMANUEL ADEBAYOR akiwa Man City: Spanish Cup (mkopo R Madrid). 

2009 ---  KOLO TOURE akiwa Man City: 1 FA Cup, 1 Premier Lge.

2010 ---  FRAN MERIDA akiwa A Madrid: 1 Euro Super Cup.

2011 ---  CESC FABREGAS akiwa Barcelona: 1 Euro Super Cup, 1 Club World Cup, 1

                Spanish Cup. 

2011 ---  GAEL CLICHY akiwa Man City: 1 Premier League. 

2011 ---  SAMIR NASRI akiwa Man City: 1 Premier League.
.


WIKIENDI NJEMAAAAAAAAAAA!!!

No comments:

Post a Comment