Saturday, August 18, 2012

BREAKING NEWS: Barcelona Yathibitisha Kamnyakua Alex Song

Barcelona wametangaza kua wamekubaliana na Arsenal kumsajili kiungo wao mahiri Alex Song, kwa ada ya uhamisho inayosadikiwa kua pauni milioni 17 jioni hii.Song, 24, alijiunga na Arsenal akitokea Bastia, mwanzoni akiwa amesajiliwa kwa mkopo kwa msimu 2005-06 kabla hajachukuliwa jumla mwaka uliofuata kwa ada ya pauni milioni 1 tu. Ingawa kulikua na maswali mengi juu ya uwezo wake, Song ameibukia na kua mmoja kati ya wachezaji wa kutegemewa Gunners.
M-Cameroon huyo aliichezea Arsenal mechi 46 msimu uliopita, lakini dirisha hili la usajili ndio hasa tetesi za kuondoka kwake zilianza, kama fullSoka lilivyowajulisha siku nne zilizopita juu ya kutakiwa kwake na Barcelona.
Kufuatia kuondoka kwa Robin van Persie kwenda Manchester United, meneja Arsene Wenger alithibitisha Song angeweza kuondoka klabuni hapo. Leo Jumamosi, baada ya Arsenal kutoka suluhu ya 0-0 dhidi ya Sunderland, Barcelona walitangaza makubaliano yamefikiwa.
Akaunti ya Twitter ya Barca iliandika: "FC Barcelona wamefanya makubaliano na Arsenal FC juu ya uhamisho wa Alex Song kuja Camp Nou.
"Song atasaini mkataba wa misimu mitano akiwa na mkataba wa kusajiliwa na timu nyingine(release clause ) € milioni 80. Siku ya Jumatatu atafanya uchunguzi wa afya na kisha atajiunga na wenzake kwa ajili ya utambulisho maalumu  wa timu huko Gamper." 
Na Arsenal pia wakaandika: "Arsenal Football Club wanathibitisha kwamba makubaliano na Barcelona juu ya uhamisho Alex Song yamefikiwa. Song atasafiri kwenda klabu hiyo ya Catalan kufanya makubaliano binafsi kakamilisha usajili."

No comments:

Post a Comment