Monday, August 20, 2012

Mchelewaji, mzembe, tabia mbovu: Sababu zilizomuondoa Song Arsenal...


Arsenal walichoshwa na tabia za  Alex Song 
Arsene Wenger alipoamua kumuuza Song kirahisi watu wengi walipatwa na mshangao, ila hiyo inametokana na kushindwa kuendelea kumvumilia kiungo huyo limeripoti gazeti la The Daily Mirror. 
Bosi wa The Gunners aliamua kumuuza Song kwa pauni milioni 17, akiwa tayari ana uhakika wa kumpata kiungo wa Real Madrid Nuri Sahin
Ila ukweli kuhusu kuondoka kwake ni kwamba klabu iliamua kumuaondoa baada ya kuendelea kuja mazoezini akiwa amechelewa, na hiyo kuchukuliwa kama dharau na uzembe na pia kutokusikiliza maelekezo ya makocha wa ulinzi kumtaka awe mkabaji zaidi badala ya kupenda kupanda na kuacha mwanya mbele ya mabeki wanne.


Song ambaye mkataba wake ulikua umalizike 2015, hivi karibuni alianza kulazimisha kufanyika kwa makubaliano mapya kuhusu mkataba wake na lengo lake liligundulika pale Arsenal walipopata taarifa kwamba Barca wanamuhitaji.

Kwa kuthibitisha hilo Song mwenyewe aliwaambia Arsenal anataka kuondoka wiki iliyopita, na klabu haikufanya jitihada zozote za kutaka kumzuia ingawa walikua na uwezo huo.


Training grounds for concern: Arsene Wenger has not been impressed with Alex Song's performances off the pitch




Mazoezini: Arsene Wanger hakua anavutiwa na tabia za song hasa mazoezini.

facebook.com/FullSoka
 Pamoja na tetesi za kutakiwa Barcelona, sababu kubwa ilikua ni tabia zake hapo nyuma na yeye mwenyewe kuomba kuondoka - wakaamua kumuuza, ingawa hapakua na presha yoyote ya kulazimika kufanya hivyo kwa mchezaji muhimu aliyeongoza kwa kutoa pasi nyingi zilizozaa magoli, pasi 11 msimu uliopita.

Barcelona walipoona urahisi walifanya mambo haraka na Arsenal sasa wapo mbioni kukamilisha usajili wa Sahin kwa mkopo wa mwaka mmoja, ingawa aina ya uchezaji wa Sahin ni tofauti na Song.

Song alikwea pipa jana kwenda jijini Barcelona kufanyiwa uchunguzi wa afya yake kabla ya kukamilisha makubaliano binafsi kwa mshahara wa pauni 70,000 kwa wiki.

Arsene alianza kutilia shaka tabia za Song katikati ya msimu uliopita, na akaanza kumfuatilia kiungo mkabaji wa Rennes Yann M'Vila .























    









     

Yann M'Vila gestures during the French cup football match Rennes against Nancy                                                                                                                                                                                 
Yann kwa Song? Arsene Wenger anamtafakari Yann M'Vila kama mbadala wa Song

facebook.com/FullSoka
Na wiki iliyopita alithibitisha uamuzi wake wa kumuuza. Wenger alisema: " Kuna sababu tofautitofauti, sitopenda kuanza na hilo kwa sasa, ila imetokea. Kesi hii ni ya mtu binafsi ila labda siku moja nitawaelezeni kila kitu.

"Ni uamuzi pekee tuliobaki nao(kumuuza) na sasa itabidi tukubaliane na hilo kwa namna sahihi.

"Natumai tunaweza. Inawezekana tukaleta mchezaji, kama hilo halitofanikiwa bado tuna viungo wengi.

"Hapa tunatengeneza wachezaji. Wote walioondoka walitengenezwa hapa ama walitengeneza jina hapa ama walikuja wakiwa wadogo sana.

Fabregas, Clichy, Adebayor, Henry, Nasri, hao wote. Song alikuja akiwa na miaka 17. Alikua na mengi sana ya kujifunza ila aliweza.

"Naamini sehemu ya klabu yetu ni kufanikisha maisha ya watu kwa njia sahihi. Ungependelea kufanikisha hilo kwa njia zilizo bora ila si mara zote hilo hufikiwa." alimalizia Wenger.

Natumai akiwa Barca atanyooka.

IDDI PILI NJEMA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

No comments:

Post a Comment