Saturday, August 25, 2012

Chelsea Wamnyakua Mnigeria Victor Moses


Chelsea wamekamilisha usajili uliokuwa na mizengwe wa Voctor Moses kutoka Wigan leo Ijumaa baada ya kufaulu uchunguzi wa afya na kukubaliana kuhusu mahitaji yake binafsi.
The Blues walishuhudia ofa zao nne zikikataliwa na Mwenyekiti wa Wigan Dave Whelan. Sakata hili lilidumu tokea msimu ulipomalizika.
Whelan aliwaudhi Chelsea kwa kuongea hadharani kuhusiana na ofa walizokuwa wakitoa kwa kile kilichotafsiriwa kama kutaka kupandisha bei iwapo timu nyingine ingejitokeza kumtaka. 
Roberto Di Matteo amefanikiwa kumpata Victor Moses baada ya ofa ya mara ya tano kukubaliwa na Wigan siku ya Alhamisi, na kuthibitisha kwamba wamekubali ofa mpya kutoka Chelsea.
Ada ya uhamisho wa Moses mwenye umri wa miaka 21 inaaminika kua takribani pauni milioni 9.

Moses: alionesha kiwango kizuri alipocheza dhidi ya Chelsea wikiendi iliyopita
"Timu ya Chelsea inafuraha kutangaza kumsajili Victor Moses kutoka timu ya Wigan Athletic," taarifa kutoka mtandao wa Chelsea umethibitisha.
Chelsea hawakusema urefu wa mkataba wa Moses, ambaye alijiunga na Wigan akitokea Crystal Palace mwaka 2010 na kiwango chake kikapanda hasa msimu uliopita.
Moses ambaye amefunga mara nane katika mechi 74 za ligi, alionesha kiwango kizuri katika mchezo wa hivi karibuni wa Ligi Kuu waliolala 2-0 dhidi ya Chelsea wikiendi iliyopita.


Ana kibarua kigumu cha kufikia kiwango cha juu Stamford Bridge
Ikiwa ni dhahiri anaonekana atakuja kuwa mchezaji hodari, Moses ana kibarua kizito cha kukuza kiwango chake kuzidi hata alichonacho sasa ili apate kudumu Stamford Brigde. 
Ugumu huo unakuja baada ya Chelsea kua na viungo wa pembeni wa viwango vya juu wanaocheza nafasi moja na Moses: wachezaji kama Eden Hazard,Juan Mata, Daniel Sturridge na Marko Marin.  
 Katika duru la kimataifa, Moses aliichezea Uingereza tokea akiwa shule mpaka kufikia kiwango cha timu ya taifa chini ya miaka 21 (U-21), ila aliamua kuichezea Nigeria baada ya Uingereza kusuasua kumuita katika timu ya taifa hilo ya wakubwa. 
Ameichezea Nigeria mechi yake ya kwanza mwezi Februari mwaka huu dhidi ya Rwanda. 
Moses ni mchezaji wa pili kusajiliwa na Roberto Di Matteo ndani ya masaa machache, baada ya kumnyakua beki wa kulia wa Uhispania Cesar Azpolicueta kwa kitita cha pauni milioni 7 akitokea Marseille ya Ufaransa.
NAKUTAKIA JUMAMOSI NJEMA!!!!!!!!

No comments:

Post a Comment