Saturday, August 18, 2012

BREAKING NEWS: Barcelona Yathibitisha Kamnyakua Alex Song

Barcelona wametangaza kua wamekubaliana na Arsenal kumsajili kiungo wao mahiri Alex Song, kwa ada ya uhamisho inayosadikiwa kua pauni milioni 17 jioni hii.



Song, 24, alijiunga na Arsenal akitokea Bastia, mwanzoni akiwa amesajiliwa kwa mkopo kwa msimu 2005-06 kabla hajachukuliwa jumla mwaka uliofuata kwa ada ya pauni milioni 1 tu. Ingawa kulikua na maswali mengi juu ya uwezo wake, Song ameibukia na kua mmoja kati ya wachezaji wa kutegemewa Gunners.
M-Cameroon huyo aliichezea Arsenal mechi 46 msimu uliopita, lakini dirisha hili la usajili ndio hasa tetesi za kuondoka kwake zilianza, kama fullSoka lilivyowajulisha siku nne zilizopita juu ya kutakiwa kwake na Barcelona.
Kufuatia kuondoka kwa Robin van Persie kwenda Manchester United, meneja Arsene Wenger alithibitisha Song angeweza kuondoka klabuni hapo. Leo Jumamosi, baada ya Arsenal kutoka suluhu ya 0-0 dhidi ya Sunderland, Barcelona walitangaza makubaliano yamefikiwa.
Akaunti ya Twitter ya Barca iliandika: "FC Barcelona wamefanya makubaliano na Arsenal FC juu ya uhamisho wa Alex Song kuja Camp Nou.
"Song atasaini mkataba wa misimu mitano akiwa na mkataba wa kusajiliwa na timu nyingine(release clause ) € milioni 80. Siku ya Jumatatu atafanya uchunguzi wa afya na kisha atajiunga na wenzake kwa ajili ya utambulisho maalumu  wa timu huko Gamper." 
Na Arsenal pia wakaandika: "Arsenal Football Club wanathibitisha kwamba makubaliano na Barcelona juu ya uhamisho Alex Song yamefikiwa. Song atasafiri kwenda klabu hiyo ya Catalan kufanya makubaliano binafsi kakamilisha usajili."
Soma zaidi ...

Picha Maalum RvP akiwa United

Photo: Can our new number 20 fire us to our 20th league title? See all the other squad numbers here http://bit.ly/TKtv4V
Van Persie kwa kusaidiwa na Sir Ferguson akionesha jezi yake number 20: je atawapa taji namba 20?

Photo: Robin van Persie shows us his team watch. For all the latest RvP content click http://bit.ly/MClsGQ
Robin van Persie na Bosi wakionesha saa maalum za Mashetani Wekundu  

Photo: Robin meets his new team mates at Carrington. For more exclusive content visit http://bit.ly/MClsGQ
Robin akisalimiana na wachezaji wenza wapya mazoezini Carrington 

Photo: "I'm proud to be here and looking forward to achieving big things” says Robin http://bit.ly/OrRpgJ. What will the Reds achieve with RvP’s goals?
"Nina furaha kua hapa na nina hamu ya kufanikiwa zaidi hapa” alisema Robin

Photo: RvP joins in his first training session. See our exclusive gallery http://bit.ly/NLN4Je
RvP akiwa mazoezini kwa mara ya kwanza. 

Photo: “Robin was desperate to come to Manchester United” says Sir Alex http://bit.ly/Q6UR0n. RvP only wanted to join the biggest club in the world…
“Robin alitaka sana kuja Manchester United” alisema Sir Alex 

Photo: Robin van Persie signs for United. Click http://bit.ly/Pqc0Ws for more RvP content
Robin van Persie sakisaini United
Soma zaidi ...

Ferdinand apigwa faini kwa kumtukana Ashley Cole Choc

Rio Ferdinand apigwa faini kwa kumtusi Ashley Cole kwenye Twitter

Beki wa Manchester United Rio Ferdinand ametozwa faini ya pauni za Uingereza 45,000 sawa na dola za kimarekani $71,000 na chama cha mpira cha England baada ya kupatikana na hatia ya kutumia lugha mbovu kuhusu beki wa Chelsea Ashley Cole.
Kitengo huru imempata na hatia kwa kumkashifu Cole akitumia lugha inayopdhalilisha kwa msemo wa maneno 'Choc ice' kwa maana mtu mweusi nje na ndani mzungu.
Ferdinand alikanusha kua sivyo hivyo ila ni kwamba maanake ni mtu feki, au mnafiki.
Siku mdogo wa Rio Ferdinand: Anton Ferdinand walipokwaruzana na John Terry  
Matamshi yaliyopeperushwa kwa mtandao wa Twitter yalitokea baada ya Ashley Cole kutoa ushahidi mahakamani dhidi ya mdogo wake Rio aliyedai kua alitukanwa na John Terry. Terry hakupatikana na hatia.
Rio Ferdinand na Ashley Cole Twitter

Bosi wa United Sir Alex FErguson anaamini adhabu aliyopewa Ferdinand inaashishia hatari ya wachezaji mastaa kutumia Twitter. 
Ferguson alibainisha wachezaji wote wa United wamezuiwa kuongelea klabu on Twitter na amewaonya wale hujiachia kwenye mitandao kua wanatafuta matatizo na chama cha mpira FA.
"Ilikua dhahiri ingetokea. alisema baada ya faini ya Ferdinand. " Wanataka (The FA) kuvuia kabisa suala hili (Twitter)."
"Kinachonishangaza ni kwamba wachezaji wengine wamekua wakitweet kwa miaka sasa na hawajawahi kuulizwa chochote na FA.
"Sijui hasa inakuwaje mtu anajihusisha na Twitter. Ila ipo na kama klabu tumetoa maelekezo kwa wachezaji kwamba hawawezi kuiongelea klabu kwenye Tweeter
"Rio ni mtu mzima ila anatakiwa kujua neno moja tu linaweza tafsiriwa tofauti - na huwezi tena kulibadilisha."
England team-mates ... John Terry, Ashley Cole na Rio Ferdinand





Soma zaidi ...

Friday, August 17, 2012

Wenger: Song naweza Uza Barca

Meneja wa Arsenal Arsenal Wenger amekubali kwamba Alex Song anaweza kua mchezaji anayefuata kuondoka klabuni hapo msimu huu, Barcelona wakiwa mstari wa mbele kufukuzia saini yake. 

Wenger ambaye kwa kawaida hua si muwazi  kwenye mambo ya kuuza na kununua wachezaji ila safari hii amesema anaweza muuza Song, ikizingatiwa kwa sasa van Persie ni mchezaji rasmi wa Mashetani Wekundu.
Arsenal hawajaamua kumuuza Song ama kumbakisha

Akijibu maswali kuhusu mechi za ufunguzi wa msimu mpya  jumamosi. Wenger alipoulizwa kama Song atakuwepo ama atauzwa alijibu : " Yote yanawezekana, ila akili yangu ipo zaidi kwenye mechi ya ufunguzi na Sunderland. Uamuzi kuhusu Song bado sijaamua."

Alipoulizwa kama kuna ofa wamepokea kutoka Barca alijubu: "Hapana, siwezi kukwambieni zaidi. Wenger alionekana kua wazi kuuza, akisifu wingi wa wachezaji wa kiungo alionao.

"Kiungo ni eneo tofauti kwa sababu tuna viungo tisa ama kumi wa kiwango cha juu," alisema. " Leo tu tuna viungo sita ama saba ambao wako tayari kwa mchezo, ukiongeza Wilshare na Frimpong ambaye yupo mbioni kurudi. Diaby ameshapona, Arteta, Cazorla, Ramsey, Oxlade-Chamberlain naye nimeamua atakua anacheza kiungo wa kati- kwa hiyo kiungo ni eneo ambalo tunaweza kufanya maamuzi yeyote bila kuathirika."
Soma zaidi ...

Vermaelen Captain Mpya wa Arsenal, Arteta msaidizi

Arsenal Wenger  amesema kwamba beki wa kati wa Arsenal na nahodha wa Belgium ndiye atakayechukua mikoba ya ukapteni ya mshambuliaji Robin van Persie aliyetimkia Man United na ataanza rasmi pindi Arsenal watapofungua pazia la Premier League siku ya Jumamosi.

EPL, Thomas Vermaelen, Arsenal v Newcastle United
Thomas Vermaelen amechaguliwa kuabadili Robin van Persie kama nahodha wa Arsenal, manager Arsene Wenger amethibitisha.

Van Persie akiwa keshakamilisha taratibu za kujiunga na Manchester United,Arene Wenger alikua tayari na jina la nahodha mpya mbele ya mechi ya ufunguzi dhidi ya Sunderland.

Mikel Arteta amechaguliwa na Wenger kua nahodha msaidizi ikiwa huu ndio msimu wake wa pili klabuni akiwa kasajiliwa kotokea Everton majira ya joto yaliyopita.
"Nahodha mpya sasa ni Vermaelen na [msaidizi wake ni] Arteta," Wenger aliwaambia waandishi wa habari. "Tuna wachezaji wengi wanaoweza kua manahodha katika timu hii."

Vermaelen alijiunga na the Gunners akitokea Ajax June mwaka 2009, na mara moja akajiimarisha na kua maarufu miongoni mwa mashabiki wa klabu yake, akifunga katika mechi yake ya kwanza (debut) dhidi ya Everton na akaendelea kufunga magoli muhimu katika msimu wake wa kwanza.

Baada ya kuwa nje kwa kipindi kirefu kutokana na majeruhi aliyokuwa nayo, nahodha huyo wa Belgium alirudi tena uwanjani zikiwa zimesalia mechi chache msimu kumalizika na alitengeneza ngome thabiti na Mfaransa Laurent Koscielny.

Arsenal watawakaribisha Paka Weusi (jina la utani la Sunderland) siku ya Jumamosi  jioni kwa majira ya Tanzania katika kiwanja cha Emirates wakitaraji kuanza vizuri na kuongeza nguvu ili wapate nafasi zaidi ya watatu waliyofanikiwa kukamata msimu uliopita wa Premier League, na Wenger anajua hiyo mechi itakuwa ngumu kwao.

Alisema: "Kwa kawaida mechi za ufunguzi hua nzito na ngumu sana, utakua mchezo wa maguvu. Tutatakiwa kutengeneza nafasi." alimalizia.

Ramadhan Kareem!!!!!!!!!!



Soma zaidi ...

Arsenal kumpa Jezi namba 10 ya van Persie Wilshere

Podolski amemuachia kiungo wa mwuingereza aliyekua majeruhi kuchukua jezi namba 10 - na ana shauku ya kuivaa kabla ya Christmas!

Christmas presence: Showing up before Santa is now Wilshere's target
Kurudi uwanjani kabla ya Christmas ndio tageti ya Wilshere 

Jack Wilshere atapewa jezi namba 10 ya mshambuliaji anayeihama klabu hiyo Robin van Persie - kwa kuonesha imani nae na kumpa moyo zaidi apone haraka.
Bosi wa Arsenal Arsene Wenger amekubaliana na hilo, ni kitu kitachompa ahueni kubwa Wilshere akiwa anapigania kupona majeraha yake ambayo yamemfanya asiweze kugusa mpira tokea msimu uliopita.
Chipukizi huyo wa kiingereza Wilshere, miaka 20, anatarajia kurudi uwanjani kabla ya Christmas baada ya kua nje ya kiwanja kwa zaidi ya mwaka kwa majeraha ya goti na misulia.
Wenger anamtaka ndiye awe fundi katikati ya kiwanja na hivyo atapewa namba hiyo  ambayo inayohusishwa na mchezaji fundi uwanjani.
Namba10 hua ina umuhimu sana Arsenal baada ya mdachi Dennis Bergkamp kuivaa,watu wa Mahusiano (PR) pia wanataka kutumia mwanya huo kukuza brandi zaidi na kuuza jezi za Wilshare akiwa ni kipenzi cha mashabiki wa The Gunners. 
Mshambuliai mpya Lukas Podolski alicheleweshwa kupewa namba mpaka sasa dhumini likiwa ni kuona kama van Persie ataondoka ama atabaki, ingawa alitakiwa kupewa ikiwa van Persie ameondoka, baada ya kujua mapenzi ya mashabiki wa Arsenal na Wilshare imebidi ajiweke pembeni, zaidi akijikita kuwazoea wachazaji wenzake na sistimu ya uchezaji ya timu.

Soma zaidi ...

Karibu Manchester! Picha za RvP akiwasili United kukamilisha usajili leo asubuhi


"Ni jambo kubwa sana kua na mchezaji mwenye uwezo wa van Persie kujiunga na kikosi chetu," amesema Fergie 

Hope they have warm hands! Van Persie arrives at Bridgewater Hospital
Van Persie akiwasili katika hospitali ya Bridgewaterkuchukua vipimo vya afya

Sir Alex Ferguson amesema Manchester United sasa wana kikundi bora cha mastaika kama kile kilichowawezesha kuchukua vikpmbe vitatu mwaka 1999.
Robin van Persie anakamilisha taratibu za usajili wa paundi milioni 24 kutoka Arsenal kwenda Old Trafford leo Ijumaa, akisaini mkataba wa miaka minne kwa mshahara wa paundi elfu 200 kwa wiki, alfajiri hii amewasili katika hospitali ya Bridgewater jijini Manchester kwa ajili ya uchunguzi wa afya.
ROBIN VAN PERSIE ARRIVES IN MANCHESTER
Heading in: wawakilishi wa United wakihakikisha Van Persie ameingia kwenye gati la Bridgewater


Na Ferguson anaamini kwamba washambuliaji wake wanne Van Persie, Wayne Rooney, Danny Welbeck na Javier Hernandez wanaweza kufikia ama kupita kabisa mafanikio waliyopata mashujaa waliochukua vikombe vitatu msimu mmoja mwaka 1999.
“Rooney na Van Persie ni wachezaji bora sana na ni jambo zuri kua nao wote,” alisema Ferguson. “kumsajili Van Persie kutatuongezea nguvu zaidi kwenye mashambulizi.
“Tukirudi mwaka 1999 tulikua na Dwight Yorke, Andy Cole, Teddy Sheringham na Ole Gunnar Solskjaer – washambuliaji bora barani ulaya kwa wakati huo.
“Ndipo tunapoelekea kwa sasa tukiwa na Wayne, Robin, Chicharito na Danny. Ni fungu la wachezaji bora sana nachoombea kwa sasa ni nipatie kuchagua combination sahihi.
Ferguson, akiongea katika uzinduzi wa ushirikiano baina ya United na kampuni ya kamali za mtandaoni Bwin, aliongeza kwamba: “Van Persie bado hajasaini, ila tumeshakubaliana ada ya uhamisho.
“Sasa yupo njiani kutokea London na tutampima afya. Nataraji kila kitu kitaenda sawa kama tulivyopanga.
“Agent wake pia yupo katika maongezi na CEO David Gill. Pia naomba, kila kitu kitakua shwari kufikia jioni.
“Nina uhakika atakua tayari kucheza mechi ya jumatatu dhidi ya Everton.”
wayne rooney robin van persie
Watch out Everton: Wayne Rooney na Robin van Persie wataanza mechi na Everton

GETTY

Hata hivyo kuna uwekano mshambuliaji mmoja wa Manchester United anaweza kujiunga na Arsenal.Click hapa ujue ni mchezaji gani.


Mashetani Wekundu: Rio Ferdinand akiwaongoza Manchester United mazoezini leo asubuhi


 Toa maoni yako kama una cha kuchangia hapo chini........Aljumaa Kareem na Mwezi Mtukufu

Soma zaidi ...

Thursday, August 16, 2012

'Hatukua na Jinsi Ilibidi lazima Tumuuze RvP': Arsene Wenger

Sir  Alex Ferguson na Robin van Persie
Bosi wa Arsenal Arsene Wenger amewaambia mashabiki wa Gunners kua hawakua na jinsi zaidi ya kumuuza Robin van Persie Manchester United.
Sir Alex Ferguson alithibitisha jana kwamba wamekubaliana na Arsenal uhamisho wa paundi milioni 24, kwa Mdachi huyo ambaye leo hii atakua anafanya uchunguzi wa afya ili kumalizia taratibu za usajili.
"Sasa yupo Manchester United, ni bahati mbaya kwetu. Uhamisho ulikamilika leo mchana," Wenger aliiambia televisheni ya Ufaransa TF1.
"Si jambo zuri kupoteza wachezaji wa kiwango kile ila alibakisha mwaka mmoja na akakataa kuongeza kwa hiyo hatukua na jinsi tena."
“read more” 
New No 10? Lukas Podolski ndiye atakayechukua jezi namba kumi.
Wenger pia alisema kwamba pesa walizopata kutokana na mauzo ya van Persie hazitotumika hivi karibuni, kwa kua ameshawanunua wachezaji wapya majira haya ya joto.
"Tumesha sajili (Olivier) Giroud na (Lukas) Podolski ambao kimsingi tuliwanunua kuziba pengo la kuondoka kwa van Persie," alimalizia.
'We had no choice': Arsene Wenger was forced to sell Robin van Persie
'We had no choice': Arsene Wenger was forced to sell Robin van Persie 
Getting shirty: Arsenal fans burn their RvP replica shirt that probably cost them upwards of £40
Baadhi ya Mashabiki wa Arsenal walionesha kukerwa kwao na kitendo cha RvP na kuchoma Jezi namba kumi aliyokua akitinga

Soma zaidi ...

Chicharito Kutimkia Arsenal?

Ni kweli Hernandez ataondoka ikiwa atakua mshambuliaji chaguo namba 4? 

 Mshambuliaji wa Manchester United Javier Hernandez, inasemekana hajafurahia zoezi zima la usajili wa van Persie.


 Gazeti la Daily Mirror linamuhusisha mshambuliaji huyo kutimkia Arsenal kwani haelewi hatma yake ya kua mshambuliaji chaguo namba nne.


 Hernandez, ambae msimu wake wa pili 2011/2012 ulikua mgumu akiwa kama mshambuliaji chaguo la tatu, inasemekana hajapendezwa na linaloonekana wazi atakosa kabisa nafasi msimu ujao na kwa habari ambazo hazijathibitishwa amemwambia wazi Ferguson anataka kuondoka. 


Wayne Rooney and Robin Van Persie
Be afraid... Rooney na van Persie wataungana kukamilisha foward lina ya Manchester United
 Wiki iliyopita Ferguson alikua ameshavunjika moyo na kuamini hawezi tena kumpata van Persie, huku akilalama Wenger anataka paundi millioni 30 kwa mshambuliaji huyo.

 Arsenal watapata paundi milioni 24 kwa mshambuliaji ambaye kama asingeuzwa basi angeondoka bure baada ya mwaka mmoja, pia Gunners wanaweza kumpata Chicharito kama taarufa ya Daily Mirror ni ya kuaminika. 


Robin atapokea mshahara wa paundi 200,000 kwa miaka minne na kua mchezaji wa pili katika historia ya Man U kupokea mshahara huo mnono.


 Hapo mwanzoni Ferguson alimlaumu Wenger kwa kujaribu kumuuza van Persie kwa klabu zingine na hataki kabisa kuongea na United ingawa ndio chaguo la van Persie. 


 Baada ya majuma ya kukwepana, inasemekana Ferguson aliwasiliana moja kwa moja na Arsene Wenger ili amruhusu van Persie kujiunga na United.


 Wenger alipinga suala hilo ila ilibidi akubali baada ya ofa ya Ferguson kufikia paundi milioni 24 kwa mchezaji mwenye miaka 29 na ambaye angeondoka bure msimu ujao zaidi akiwa na rekodi mbovu ya kuumia. 


 Mashetani wekundu bila shaka watakua na ngome kali ya mashambulizi kwa kuwa na washambuliaji wawili walioongoza kwa ufungaji Premier League ikiwa msimu uliopita kwa pamoja walitikisa nyavu mara 71 kati yao. 


 Je wadhani Chicharito ataondoka? kama sivyo nini hatma yake ikiwa haafiki kua chaguo la nne?
Soma zaidi ...

Breaking News: Robin van Persie atua Manchester United

Cheers to jeers: Robin van Persie atarajie kuzomewa na mashabiki wa Arsenal ila ni furaha kwa Manchester United 

Mshambuliaji wa Arsenal striker Robin van Persie mwishowe amepata ruksa ya kuungana na Wayne Rooney Old Trafford. 

Arsenal wamethibitisha kukubaliana ada ya uhamisho juu ya mchezaji huyo na mahasimu wao wakubwa Manchester United.

Mwanasoka huyo aliyefunga jumla ya magoli 30 season iliyopita atasafiri kwenda Manchester siku ya Alhamisi kwa ajili ya makubaliano binafsi na kukamilisha uchunguzi wa afya kabla ya kutia saini.

"Arsenal Football Club inathibitisha kwamba imekubali kumuhamisha Robin van Persie kwenda Manchester United," imeandika website ya Gunners.

Van Persie, ambaye alieleza wazi nia yake ya kuondoka Emirates Stadium, anajitayarisha kusaini mkataba wa miaka minne kuwepo Old Trafford kwa paundi milioni 24, hiii ni kutoka kwa bosi wa Arsenal  Arsene Wenger. 

Mdachi huyo inavyoonekana ndiye atakayeongoza ngome kali ya mashambulizi ya Mashetani Wekundu, ikizingatiwa Wayne Rooney alimaliza nyuma van Persie kwa ufungaji akitikisa nyavu mara 27 msimu uliopita. Mashetani Wekundu pia wana chipukizi Danny Welbeck na Javier 'Chicharito' Hernandez kama washambulizi.

Sir Alex Ferguson inaonekana emefanikiwa kumpata mchezaji aliyemtamani kwa kipindi kirefu kwa kuwapiku majirani zao na mahasimu wakubwa Manchester City na Juventus kupata saini ya van Persie, pia wameshawaweka kibindoni chipukizi kutoka Crewe Nick Powell na kiungo wa kijapani Shinji Kagawa.
Soma zaidi ...

Tuesday, August 14, 2012

Liverpool yamnyakua Joe Allen

Joe Allen: Akithibitisha kujiunga na Liverpool
Liverpool imekamilisha kumsajili kiungo wa kati wa kimataifa Joe Allen wa Wales.
Allen, mwenye umri wa miaka 22 alikamilisha usaili wa kimatibabu siku ya Ijumaa.
Anakuwa wa pili kusajiliwa na meneja wa Liverpool Brendan Rodgers baada mshambuliaji wa kimataifa kutoka Italy Fabio Borini.
''Najisikia vizuri sana. Kila mtu anajua historia ya club hii, ni club kubwa sana, na ninafurahia kujiunga nayo,'' aliiambia wavuti ya club hiyo.
"Mapenzi ya mpira waliyo nayo watu hapa ni kitu ninachoshirikiana nao na ninataka kuwa sehemu yake.
"Nina shauku ya kuwa sehemu ya miaka ijayo ya mafanikio kwa timu ya Liverpool."

Rodgers anaamini Allen atakuwa kiungo muhimu kumuwezesha kuleta mtindo wake wa uchezaji katika timu ya Liverpool.
"Nimefurahi sana sana kwamba Joe amefanya uamuzi wa kuja kujiunga nasi katika safari hii," amesema Rodgers.
"Joe ni mchezaji ambaye uwezo wake unaweza kutumika katika eneo lolote katika timu hii. Uwezo wake wa kutawala na kumiliki mpira ni kitu muhimu katika juhudi zetu za kupata mafanikio uwanjani''.
CHANZO: BBC
Soma zaidi ...

Jack Rodwell aenda Manchester City

Jack Rodwell kwenye ofisi za Man City

Manchester City imekubali kumsajili Jack Rodwell kutoka Everton kwa kitita kilichowekwa kuwa siri.
Kiungo huyo wa kati wa miaka 21, atafanyiwa usaili wa kimatibabu siku ya Jumapili.
Rodwell, anayepewa thamani ya pauni milioni kumi na tano na Everton, wiki iliyopita alitajwa na Roy Hodgson katika kikosi cha England katika mechi na Italy siku ya Jumatano.
City kwa sasa hawana Gareth Barry kutokana na jeraha la mguu na pia hatma ya Nigel de Jong bado inabakia kuwa na utata.
Meneja wa Manchester City Roberto Mancini amesema: "Tunafikiria Jack Rodwell ni mchezaji mzuri na wa umri mdogo. Atakuwa kiungo wa kati muhimu kwa timu ya Taifa ya England na kwetu pia. Tunahitaji mtu ambaye anataka ushindi, mwenye mbinu nzuri na mchezaji bora kwa muda mrefu ujao."
Siku ya Ijumaa, Mancini alisema hakuwa na furaha kuona Club hiyo ikiwa inasitasita kununua wachezaji wapya msimu huu wa majira ya joto.
Rodwell ndiye mchezaji pekee wa juu kuingia Manchester City msimu huu wa majira ya joto, ingawaje club hiyo inasemekana kuwa na mpango wa kuwahamisha mshambuliaji wa Arsenal Robin van Persie na Daniel Agger wa Liverpool.
Rodwell ataongeza ufanisi katika sehemu ya kati ya City ambayo imedhoofishwa kutokana na kutokuwepo kwa Barry wa England na utata juu ya De Jong kuhusu mkataba mpya.
De Jong mwenye umri wa miaka 27, yuko katika mwaka wa mwisho wa mkataba wake wa sasa na ananyemelewa na Bayern Munich.
Rodwell aliibuka kupitia timu ya vijana ya Everton baada ya kujiunga nayo akiwa na umri wa miaka saba.

CHANZO: BBC
Soma zaidi ...

Sunday, August 12, 2012

Kama Alex Song Hatobadilika, Auzwe Barca

Najua sitowafurahisha mashabiki wa Arsenal ila kwa nionavyo mimi Arsenal wanahitaji Kiungo Mkabaji wa hali ya juu, swali  hapa ni je Song ni kiungo mshambuliaji ama mkabaji?
Alex Song; je hufuata maelekezo ya Arsene Wenger? 
Baadhi ya mashabiki wa Arsenal wanaamini ni Song ni mtaalam anayeweza kufungua beki pinzani na ni kati midfielders bora Ulaya.
Wengine hamuona kama ni mchezaji asiye makini na ulinzi na hukosa nidhamu ya ulinzi na kupenda zaidi kupanda mbele.
Kwa fikra zangu sikuwahi dhani Song angekuja kua mchezaji alivyo sasa. Kamwe sikuweza dhani kama angeweza kufanikiwa akiwa Arsenal. Improvement aliyopata ni ya hali ya juu, pongezi kwake na pia Arsene Wenger. Hata Wenger anakiri anashangazwa na Song alivyokua kimpira kulinganisha na alivyokua.
Song bila shaka ame-improve kwa kiwango cha kustaajabisha, tangu mchezo dhidi ya Fulham mwaka 2006 wakati alipotolewa na Wenger kipindi cha mapumziko kwa kuvurunda na baada ya miezi miwili iliyofuata kupelekwa kwa mkopo Charlton. Kwa wakati ule nilidhani ndio ulikua mwisho wake na asingeweza tena kucheza Premier League.
Alex Song akimkaba Carlos Tevez... je hii inatosha? 
Song sasa ni moja kati ya majina ya kwanza kabisa kwenye list ya Arsene Wenger apangapo timu, tokea kua mchezaji wa hovyo mpaka mchezaji anayezivutia timu kubwa Ulaya, ikiwamo Barcelona . Nionavyo mimi si kama wanamtaka kwa uwezo wake wa ukabaji.
Song anapenda kupanda mbele ni dhahiri, na msimu uliopita ameweza kutoa pasi nyingi zilizozaa magoli matamu na hasa kumtafuta Robin van Persie.
Mfano pasi alizomtolea Van Persie dhidi ya Liverpool na Everton ndizo pasi bora zaidi Premier League msimu uliopita. Amemaliza akiwa wa nne kwa kutoa pasi za kuzaa magoli, nyuma ya David Silva, Antonio Valencia na Juan Mata - na akiwa sawa na Emmanuel Adebayor - kwa assists 11.
Ila kwa mara ya kwanza alipoanza kupata namba ya kudumu Arsenal, haikua kwa uwezo wake wa kushambulia. Ilikua kwa uwezo wake wa kusaidia mabeki wanne wa mwisho(kukaba).
Hili ndilo hasa litakalomfanya Arsene Wenger afikirie mara mbilimbili juu ya kumuuza ama kumbakisha. Barcelona wamekua wakimvizia na wanaweza wakatoa ofa.
Song ana mkataba na Arsenal mpaka 2015. Arsenal hawana ulazima wa kumuuza na hata Song hajadhihirisha kama anataka kuondoka.
Kama akiuzwa, utakua ni uwamuzi wa Arsenal. Na si pande nyingine yoyote.
Na fikra zanijia kwamba Wenger anaweza muuza Song hasa ikiwa atakua na uhakika wa kumnasa Yann M'Vila.

Yann M'Vila: aweza kua mbadala wa Song. 
Arsenal wamemfuatilia kiungo huyu wa Rennes kwa muda mrefu sasa. Ila anajulikana kwa hulka mbovu hasa nje ya uwanja zilizowafanya Arsenal kupunguza mshawasha wa kumtaka kipindi cha majira ya joto. Hata hivyo, kama Song atauzwa basi mshawasha utarudi upya.
Thamani yake ni kati ya paundi za Uingereza milioni 10 mpaka 15, ila kwa vurugu na tabia zake Rennes wanaweza kumuuza hata kwa paundi milioni 10.
Pia sio siri kwamba Arsenal wanamkodolea macho mchezaji wa Real Madrid na kiungo wa Kituruki Nuri Sahin, na watazidisha juhudi hasa kama Song ataondoka hii summer.
Sahin ni hazina hasa, uchezaji wake ni tofauti na Song ila atawaongezea nguvu na machaguo zaidi kwenye nafasi za kiungo ambazo wamekua wakionekana kukosa cover za kuaminika kwa misimu ya hivi karibuni. Wanatakiwa kununua beki mwingne kwani Bacary Sagna atakosa mechi za mwanzo za msimu unaoanza punde.

Picha ya mfano Nuri Sahin akiwa ndani ya uzi wa Arsenal.  

Ila kwa nionavyo mimi, mpaka kufikia September 1(deadline day) Song atakua bado ni mchezaji wa Arsenal. Ila hili si uhakika.
Sawa na, Robin van Persie bado haijaeleweka vizuri. Si haba akaondoka dakika za mwisho ama akawepo.
Mashabiki wa Arsenal kwa mara ya kwanza tokea miaka 7 iliyopita wanamatumaini mepya kupitia manunuzi ya Santi Cazorla, Olivier Giroud na Lukas Podolski na hili litamfanya van Persie afikirie mara mbilimbili.
Santi Cazorla: je atafanya RvP abadili mawazo?

Kwa Manchester United wanaonekana watarudi tena na ofa mpya kwa Arsenal juu ya kumnyakua van Persie . Manchester City na Juventus wameshatoa ofa ambazo zilitupiliwa mbali.
Nadhani hata kama van Persie atauzwa, Arsenal wapo kamili kwa karibia idara zote. Van Persie - wapenzi wa Arsenal wakubali wasikubali - aliwabeba dhahiri kwenye baadhi ya michezo msimu uliopita. Sasa wana machaguo zaidi kwa ushambulizi.
Kama Arsenal wakimuuza Song na kumsajili M'Vila hapo kiulinzi watakua imara zaidi, kwa mawazo yangu. Pia wana Mikel Arteta na Cazorla kwenye kiungo. Jaalia, Jack Wilshere nae arudi mapema.
Ila kila timu inahitaji mhimili. Song ni lazima arudi kua imara na mwenye nidhamu katika msimu huu. Je ana ufundi tosha wa kumfanya kucheza Barcelona? Hilo jibu wewe.
Assists zake ni za kuvutia ila hili si jukumu lake kugawa mipira ya mwisho. Kama hatozingatia kulinda zaidi ya kupanda mbele na kuwaacha mabeki wakiwa wazi kwa counter attacts, basi Arsenal wamuuze na uangaliwe ustaarabu mwingine.

Premier League assists kwa msimu 2011-12

David Silva, Manchester City -15
Antonio Valencia, Manchester United - 13
Juan Mata, Chelsea - 13
Alex Song, Arsenal -11
Emmanuel Adebayor, Tottenham -11
Gareth Bale, Tottenham - 10
Nani, Manchester United -10
Samir Nasri, Manchester City -9
Stephane Sessegnon, Sunderland - 9
Robin van Persie, Arsenal - 9
Sergio Aguero, Manchester City - 8
Ryan Giggs, Manchester United - 8
Theo Walcott, Arsenal - 8
Toa comments zako hapo chini............... Mpaka muda mwigine. Ramadhan Kareem.


Soma zaidi ...

Sir Ferguson Awalaumu Arsenal! Mmmh


Hii si haki! Sir Alex Ferguson awalaumu Arsenal kuhusu Van Persie

Inapendeza kumuona Sir Alex Ferguson anapodai Arsenal hawamtendei haki juu ya Van Persie.
Fergie haelewi kwa nini Arsenal wamekua hawamtendei haki ili aweze kumnyakua mshambuliaji wao hatari kwa paundi 15 million. “Tumejaribu sana ila hakuna mafanikio. ni vigumu kuelewa kwa nini wanakua wagumu na kuendesha mambo yao kwa njia hii,” alinena.
Ukiachilia kusema kwamba kama Arsene Wenger angejaribu kumsajili Wayne Rooney kwa pesa kiduchu si tu kwamba naye(Ferguson) asingewaelewa Arsenal bali asingetoa ushirikiano wa aina yoyote ile kufanikisha suala hilo.
Acha Rooney, Fergie pia ana hasira kwa kumkosa Lucas Moura amabye amechagua PSG na si Manchester United, na anataka kujua kwa nini soka limekua ovyo: “Sielwei na ni maajabu klabu inaweza lipa paundi milioni 35.5 kwa mtoto wa miaka 19,” alisema.
Kama kumbukumbu zangu ziko sahihi nakumbuka, mwaka 2004, Fergie alitoa paundi milioni 28 kwa ajili ya kumnyakua Wayne Rooney.
Ukitumia hesabu za uwiano wa Mabenk ya Uingereza (Infation Aspect), paundi milioni 24 alizotoa kwa Wayne Rooney kipindi hicho ni sawa na paundi milioni  36.3 kwa pesa za sasa. Rooney akiwa na miaka 18 kipindi hicho.
Fergie. Kwa kweli ni ajabu.

We waonaje juu ya hili, toa maoni yako hapo chini!!!!!!!!!!!
Soma zaidi ...