Saturday, September 1, 2012

Picha: Jezi Mpya za Timu Zote za Premier League 2012/2013


Hizi ndizo jezi mpya za nyumbani na ugenini za timu zote zinazoshiriki Premier league 2012/2013

Arsenal

NYUMBANI



Nadhani nike msimu huu wamewatendea haki Arsenal, jezi nzuri rangi ngeni hapa ni bluu ila pia imetokea vizurit.

UGENINI

Mmmh! Sina uhakika na hizi, rangi ya zambarau?


Manchester United

NYUMBANI

Premier League kits 2012/13: in pictures
Baadhi ya mashabiki nilioongea nao wana mawazo tofautitofauti, illa wengi wanaipenda.

UGENINI

My fav! Moja ya kazi nzuri za Nike msimu huu, inapendeza.

Manchester City 

NYUMBANI


Mabingwa wapya! kama hautoiangalia kwa makini hautoona tofauti na jezi za msimu uliopita, kama kawa rangi yao ni nzuri.

UGENINI



  • Sare jezi zao za juu na za chini, ningependa zaidi kama zingekua bukta nyeusi. Maroon ni rangi nzuri.

Stoke City

NYUMBANI NA UGENINI


Wazee wa kutupia na mipira ya juu. Kama Barca! jezi zao za juu za ugenini labda zitawalazimu msimu huu wacheze mpira wa chini kama Barcelona.

Newcastle 

NYUMBANI


Pundamilia kama kawa, ila nyeupe imechukua nafasi kubwa ila kuanzia kiunoni ni nyeusi mpaka kwenye 

Newcastle 

UGENINI




Nzuri kuliko za ManCity ila hata wangetumia za msimu uliopita wangependeza pia na walikua na bahati nazo.

Chelsea

NYUMBANI
Kutoka mistari mweupe msimu uliopita mpaka mistari ya dhahabu! Na soksi nyeupe? Si mbaya.

UGENINI


Si mbaya ila si kawaida timu za Premier League kuvaa jezi za aina hii (Argentina?): Goodluck Torres umependeza

Liverpool

NYUMBANI

Premier League kits 2012/13: in pictures
Zinaonekana simpo, na kola zimekua kama polo shirts, Zipo kama jezi za mazoezini na si za mechi. Hata hivyo .kama wakifanikiwa kuingia 4 bora zitapendeza Champions League.


UGENINI 1


UGENINI 2

Premier League kits 2012/13: in pictures

Kuna jezi zingine unaweza ukaziona si nzuri lakini zikawa za kupendeza uwanjani..........Tusubiri hii itakavyoonekana

Swansea 

NYUMBANI

Garry Monk, wingers Nathan Dyer and Scott Sinclair and striker Danny Graham.


UGENINI

Wales international Ashley Williams was hand to launch the new patriotic number, alongside team-mates Jazz Richards, Neil Taylor and Joe Allen. -Premier League kits 2012/13: in pictures



Everton

NYUMBANI

Looking pretty Retro: Ila hilo li-block jeupe ni kubwa sana.

Everton UGENINI

Wigan

NYUMBANI



Wigan UGENINI


Norwich

NYUMBANI
Premier League kits 2012/13: in pictures

Norwich UGENINI


Iko poa..........timu nyingi zimechagua jezi nyeusi za ugenini msimu huu.

Tottenham

NYUMBANI NYEUPE NA UGENINI DARK BLUE
Premier League kits 2012/13: in pictures

QPR

NYUMBANI NYUMBANI NA UGENINI
Premier League kits 2012/13: in pictures
Nimependa kola ya V , Si mbaya.

Aston Villa

NYUMBANI NA UGENINI


Siku zote jezi ya nyumbani hua haionekani kubadilika kwa Aston Villa, nimezoea kuiona kwa hiyo si mbaya.

We glow in the dark, we glow in the dark...a bold departure from the traditional white Aston Villa away kit. Fans are already being encouraged to support 'Lambert's Limes' away from home
Kuna wakati marefa huvaa jezi za rangi hii, rangi kali machoni.

Southampton (NYUMBANI - NYEKUNDU) / (UGENINI - UGENINI)



Fulham 
NYUMBANI

Jezi yz juu kama jezi za baseball, ok tutaona.


Fulham UGENINI

Hrede Hangeland - Premier League kits 2012/13: in pictures
Hii si jezi za Wolverhampton, sijui kwa nini wamewaiga wakati wenzao walishuka nazo..

Reading 

NYUMBANI



Reading UGENINI


Zinanikumbusha jezi za Sweden ila ziko poa

West Brom 

NYUMBANI



UGENINI


Nimeipenda hii

West Ham

NYUMBANI


West Ham UGENINI


Siku Njema!!!!!!!!!!

Soma zaidi ...

Mancini Avunja Rekodi ya Usajili Mwaka Huu, Alalamika Hajaridhika!

Roberto Mancini amekuwa mwenye kulalamika juu ya usajili ulivyokwenda kwenye klabu yake ya Mancester City licha ya kutumia pauni milioni 52 kwa kununua wachezaji wapya watano katika majira haya ya usajili.


City wamewasajili Javi Garcia pauni milioni 16, Matija Nastasic pauni milioni 12, Scott Sinclair pauni milioni 6, Maicon kwa pauni milioni 3 na Jack Rodwell aliyemnunua mapema kwa pauni milioni 15.

Mancini alilalamika City wameshindwa kupata wachezaji chaguo la kwanza aliokuwa akiwataka yeye - akiwakosa Robin van Persie, Eden Hazard, Javi Martinez na Daniel De Rossi.

Alilalama: " NI vigumu kufanya kila kitu katika wiki moja ama siku kumi.
"Ligi ilipokwisha nilikaa na Bodi. Tuliongelea kuhusu wachezaji niliowataka ila mara nyingine ni vigumu kupata wachezaji wote unaowataka.
Unabidi uwe na chaguo mbadlala Ila kwa wachezaji tuliowapata, nimefurahi"


Mancini akiwa na winga mpya aliyemnunua Scott Sinclair kutoka Swansea
Mancini alitumia muda mwingi wa kipindi cha usajili kumlaumu Brian Marwood Mtawala wa Soka City kuhusu kutojishughulisha na kuwanunua wachezaji aliowapendekeza.

Waliowakosa:mchezaji kutoka Arsenal van Persie alikwenda Man U kwa pauni milioni 24, Hazard akijiunga na Chelsea kwa pauni milioni 32, Martinez akaelekea Bayern Munich kwa pauni milioni 32 pia na De Rossi akibakia Roma.

Ameambulia mlinzi wa kati Nastasic(19) akiitwa 'Nemaja Vidic Mpya'  kutokea Fiorentina, winga Sinclair (23) akitokea Swansea, M-brazili Maicon(31) kutokea Inter Milan.

Na kiungo mkabaji, Garcia (25) muda mfupi kabla dirisha la usajili kufungwa, atachukua nafasi ya Nigel de Jong aliyeuzwa AC Milan kwa dau la pauni milioni 5.

WIKIENDI NJEMAAA!!!!!!!!!
Soma zaidi ...

Droo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Yalivyopatikana 2012/2013, Iniesta Mchezaji Bora 2011/2012 Ulaya



Mabingwa watetezi wa Ligi kuu ya England Manchester City watachuana na mshindi wa mara tisa wa mabingwa wa Ulaya Real Madrid katika hatua ya makundi ya Ligi ya mabingwa wa Ulaya.
Timu ya Roberto Mancini itachuana pia na Ajax pamoja na Borussia Dortmund.
Mshindi wa hivi sasa wa Ligi hiyo Chelsea anaanza utetezi wa taji lake kwa mchuano dhidi ya Juventus, huku Celtic ikiwa imepangwa kuminyana na Barcelona katika kundi G.
Manchester United inapambana na Galatasaray, Braga na FC Cluj huku Arsenal ina Schalke, Olympiakos na Montpellier kwenye kundi lao la B.
Chelsea, iliyoibwaga Bayern Munich kupitia mikwaju ya peneti katika fainali iliyochezwa ndani ya uwanja wa Bayern msimu uliopita hivi sasa inakabiliana na upinzani wa Shaktar Donetsk kutoka Ukraine na FC Nordsjaelland ya Denmark na Juventus.
Pamoja na Barcelona, Celtic ina mlima wa kusafiri kwenda Benfica na pia safari ndefu kuelekea Spartak Moscow lakini macho ya wengi yataangazia michuano yao miwili dhidi ya washindi wa Ligi ya mabingwa wa mwaka 2011.
Kibarua cha Manchester City kimefanywa kua kikali sana kwa sababu ya vipimo vya UEFA kulingana na jinsi klabu hio ilivyoweza kushiriki mashindano ya Ulaya msimu uliopita na kuonekana kuwa kiwango chake ni cha chini, kwa hiyo Man.City inakabiliwa na kazi kubwa.
Msimu uliopita ilipopangwa na klabu iliyomaliza kwenye fainali Bayern Munich, Napoli ya Italia na Villarreal ya Uhispania mabingwa wa England walishindwa hata kufikia hatua ya kuondoana ikiwa ni mara yao ya kwanza kushiriki mashindano haya.
Orodha ya makundi:
Kundi A
Porto, Dynamo Kiev, Paris St Germain, Dinamo Zagreb

Kundi B
Arsenal, Schalke, Olympiakos, Montpellier

Kundi C
AC Milan, Zenit St Petersburg, Anderlecht, Malaga

Kundi D
Real Madrid, Manchester City, Ajax, Borussia Dortmund

Kundi E
Chelsea, Shakhtar Donetsk, Juventus, FC Nordsjaelland

Kundi F:
 Bayern Munich, Valencia, Lille, BATE Borisov

Kundi G:
 Barcelona, Benfica, Spartak Moscow, Celtic

Kundi H
Manchester United, Braga, Galatasaray, CFR Cluj

Arsenal imepangwa katika timu nane bora kutokana na kile UEFA ilitaja kama muendelezo wa kufanya vizuri katika mashindano yaliyopita.
Mabingwa watetezi Chelsea, Barcelona, Real Madrid, Manchester United, Porto na AC Milan ni miongoni mwa vilabu vikuu na hivyo vimewekwa katika droo kwa hadhi yao ya kua vilabu bora barani Ulaya.
Kati ya vilabu 32 vilivyopangwa katika droo hii 12 vimewahi kushinda na timu tatu ndipo zimeingia kwa mara ya kwanza.
Messi, Iniesta na C.Ronaldo muda mfupi kabla ya kutangazwa mchezaji bora wa Ulaya 2011/12, MOnaco-Ufaransa
Wakati huo huo mchezaji wa Barcelona Andres Iniesta amechaguliwa kuwamshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa Ulaya kwa msimu 2011/2012 baada ya kuwapiku  Christiano Ronaldo(Real Madrid) na Messi(Barcelona)


SIKU NJEMA!!!!!!!!!!!!!!
Soma zaidi ...

C. Ronaldo - Aina 10 za Ushangiliaji Wake na Anachomaanisha


Christiano Ronaldo amefunga magoli ya kila aina msimu uliopita. Kuna mpenzi wa FullSoka ametaka nimuelezee aina fulani ya ushangiliaji wa Ronaldo, hapa nitatumia fursa hii kuelezea aina 10 maarufu za ushangiliaji wake.

"The Silencer"
1. "The Silencer" huweka kidole cha shahada  katikati ya mdomo wake: huu huwa ni ujumbe kwa mashabiki wa timu pinzani na humaanisha sasa wanyamaze baada ya kuwa wameishangilia sana timu yao ama waliokuwa wanambeza. 

Mfano ni mechi ngumu kati ya Real na Atletico Madrid kombe la Copa Del Rey robo fainali ya pili baada ya kufunga bao la ushindi.


"The Thumb Sucker"
2. "The Thumb Sucker" huweka kidole gumba chake kimywani huku akikinyonya. Hua ni ishara kwa mwanawe wa kiume aliye na umri chini ya mwaka mmoja aitwaye Christiano Ronaldo "Junior".




"The Claw" 
3. "The Claw" ishara ya makucha yaliyotayari kushambulia au ishara ya kupanda kuelekea juu. Hii hua ni ishara kwa mwanae(CR Junior) na girlfriend wake(Irina Shayk): pindi anapokua na mtoto wake ishara hii ndiyo humfanya mtoto huyo afurahi hata kama alikua analia.

Aliigundua pale alipomuiga mtoto wake huyo baada ya kumuona akijaribu bila mafanikio kuparamia kingo za kitanda chake cha kitoto ili atoke. 

Naye alipomuiga kwa kuonesha ishara ya "The Claw" mtoto ikawa kicheko, basi tokea hapo naye imekua ni ishara kuu kila anapofunga goli.

             
Akimuonesha "The Claw" girlfriend wake Irina anayeonekana kaboreka Barnebeu, labda akidhani nae atacheka kama mwanaye, ni siku Real Ilipoifunga Vallecano 6-1 ye akifunga Hat-Trick 



Ronaldo akijinyonganyoka wala huwezi kuita kucheza mziki 
4. "The Dance" Hunyoosha mikono mbele huku akijinyonganyonga na kurukuruka. Kama jina lenyewe lilivyo "kucheza mziki", hii ishara hua ni kwa wachezaji wenzake, aliifanya mara moja tu nadhani baada ya kugundua ye si mchezaji mzuri wa muziki basi hata hakuirudia tena.



"The Fist Anger" 
5. "The Fist Anger" Hukunja ngumi mikono yote miwili kisha huku akipiga mayowe hunyanyua mkono wa kulia huku akiwa kakaza mwili. Hii hua ni ishara kwa mashabiki, na wachezaji wenzake hasa anapofunga baada ya mchezo kua mgumu. Ishara hii huonesha uwezo, nguvu na hasira. Picha hii ilichukuliwa kati ya mchezo dhidi ya Rancing Santander uliopigwa Santiago Bernabeu.


"The Deaf" 
6. "The deaf" - Christiano Ronaldo hua anatukanwa sana katika viwanja vingi vya ugenini hasa Nou Camp. Ushangiliaji wa kuweka kiganja kilichofunguka nyuma ya sikio hua ni kwa mashabiki pinzani, tofauti na "The Silencer" ambayo huwataka wafunge midomo hii hua anaashiria hajasikia matusi yao kwa ishara kwamba wazidishe sauti.

"The Sliding Machine" 
7. "The Sliding Machine" Ishara ya mambo kuwa rahisi na  kufurahia mchezo hasa anapofunga magoli mengi. Urahisi huo huufananisha na kuteleza kwenye zile tube za kuchezea watoto (Aqua Splash). 

"From Ronaldo To Ronaldo"

8. "From Ronaldo To Ronaldo"  Ishara ya kushika kichwa na kuvuta kumbukumbu ya jambo flani. Hii anaashiria kumtunuku Ronaldo De Lima na kukumbusha ukubwa wa jina "Ronaldo", Ronaldo De Lima ndiye hasa aliyeanzisha ushangiliaji huu akiwa pia Real ila akimaanisha kitu tofauti. Kwa CR7 hufanya hivyo kuashiria ukubwa wa jina lao hilo -Ronaldo- 

"The Kindergatten"  
9."The Kindergatten" Baada ya kufunga humvuta mkono mchezaji mwenzake aliyempa pasi ya goli kwa mfano wa kumuongoza njia ama kumsaidia kuvuka barabara mtoto wa chekechea. Picha hii ni pale alipofanya na DiMaria kwenye mashindano ya UEFA Champions League, dhidi ya Ajax.

"The Claw Mirror"   
10. "The Claw Morror" - Christiano hurudia ishara ya "The Claw" ila mara hii hufanya kwa msaada wa mchezaji mwenza huku wakiwa wanaangaliana. Hii ilikua mechi dhidi ya Getafe. Kama maana ya kwanza ni kuonesha furaha na kumshirikisha mwenza wake kwenye furaha yake.


 Ok, sasa wajua hua anamaanisha nini...................ukiwa na swali tuma kwenye email iliyopo hapo juu (fullsoka@gmail.com) nasi tutajibu bila kuchelewa.

Kazi Njema!!!!!!!!!
Soma zaidi ...