Sunday, August 26, 2012

Song: Mimi si Mzembe, Arsenal Walinidanganya kwa Miezi Nane


Leo Alex Song amejibu shutma alizotupiwa baada ya usajili ulioshangaza wa pauni milioni 15 kujiunga na Barcelona.Kiungo huyo wa Cameroon amefanya mahojiano ya kwanza tokea alipojiunga na Barca na akaelezea kinagaubaga:
  •  Alivyokuwa anataka kubakia Arsenal
  •  Alivyokuwa anapigwa kalenda kila alipojaribu kufanya mazungumzo ya kurefushwa mkataba.
  •   Alivyojisikia juu ya shutma kuwa alikuwa na mzembe na mchelewaji mazoezini.


Song alisema: 
"Nilipoaamka na kusoma hizo habari nilishangaa na nilivunjika moyo. Naipenda Arsenal, sijawahi kutaka kuihama.

" Nilikuwa tayari kujifunga katika klabu ile. Kitu nilichotaka ni maongezi kuhusu mkataba mpya lakini kila mara ilipotakiwa tukae mezani, klabu ilihairisha. Walikuwa wakinidanganya.
"Nilitaka mkataba mpya wa miaka mitano. Mwishowe niliupata Barcelona."

Song alichezea Arsenal jumla ya mechi 197 tokea alipojiunga kwa ada ya uhamisho pauni milioni 1 kutoka klabu ya Bestia ya Ufaransa mwezi August 2006.



Msimu uliopita alicheza michezo 46, akaongoza kwa kutoa pasi zilizozaa magoli na akawa wa pili nyuma ya van Persie " Mchezaji Bora wa Msimu Arsenal" kwa kura amabazo hupigwa na mashabiki wa Arsenal duniani kote.


Wachezaji wote hao wawili wamekitoa, RVP akijiunga na Manchester United Song akitimkia Barcelona.

Song alikuwa katikati ya mkataba wake aliokuwa analipwa pauni 55,000 kwa wiki. Kiungo huyo kwa mara ya kwanza aliwaomba Arsenal kukaa ili waongeze mkataba nwezi Novemba. Akitaka kuonesha imani yake kwa klabu wakati wachezaji kama Fabregas na Nasri wakiondoka.

Aliambiwa asubiri mpaka Mwaka Mpya, Januari aliingia na kuishia na Arsenal hawakuonesha nia ya kutaka kuongea kuhusiana na mkataba wake na wakasogeza mbele kikao hicho kuwa mwezi Machi ama Aprili.

Waliendelea kuahirisha mara zote na akaambiwa asubiri mpaka mwisho wa msimu - msimu ukaisha na mashindano ya Ulaya yakaanza wakiwa bado kimya.

Mwishowe klabu ilimwambia itamfahamisha lini watakaa kuongelea mkataba wake, hivyo aache kuuliza uliza.


Alex Song Newly signed FC Barcelona player Alex Song (L), Cesc Fabregas (C) and Jordi Alba of FC Barcelona look on prior to the Joan Gamper Trophy friendly match between FC Barcelona and Sampdoria at Camp Nou on August 20, 2012 in Barcelona, Spain.
Song akiwa Barca na rafikiye Cesc 

Song aliongeza: " Nilijaribu kwa miezi nane kuongea nao kuhusu mkataba mrefu ila klabu ilikuwa ikiahirisha kila wakati, na waliniambia 'Una miaka mitatu imebakia"



"Sikuongelea suala la pesa nilichotaka ni kukaa nao na kuongelea mkataba mpya - nilitaka nimalizie mpira wangu kwenye klabu hiyo niliyokuwa naipenda.

" Nikiwa sina hili wala lile, Barcelona wakaja wakinitaka.
"Klabu bora duniani, Barcelona walinitaka na wakawa tayari kunipa mkataba wa miaka mitano niliokuwa nautaka Arsenal."

Wakati huo Arsenal walikuwa wameshampa ahadi nyingine ya kuongea nae Mwezi wa tisa ama wa kumi, baada ya dirisha la usajili. 

Hapo akaona hana sababu kukataa ofa ya Barca wakati hana uhakika kama Arsenal wangempa mkataba anaoutaka.

Song na familia yake 

Song alisema: "Barcelona walijitayarisha kunipa mkataba wa miaka mitano sawa na ule niliokuwa nauomba Arsenal kwa miezi nane.
"Pindi timu bora inapotambua uwezo wako ina maana una fanya vitu vizuri. 

Ofa ya Barca kwa Arsenal ilikubaliwa haraka, ila Song alikasirika mara habari zilipoanza kuzagaa - kutoka vyanzo vya Arsenal - vikimshutumu kuwa mzembe, tabia mbovu na kuchelewa mazoezini.


Aliongeza: Nimehuzunishwa. Shutuma hivi ni za kuumiza, za kuniharibia jina.

"Namuheshimu sana Arsene Wenger, Nilimpenda kama baba ni kocha wa hali ya juu.

"Yeye ndiye aliyefanya mimi niwe hivi na nina deni kwake.

Barcelona wameona wamepata bahati ya mtende, kwani wamemuwekea kifungu katika mkataba wake wa ada ya uhamishi wa pauni 63 milioni kama kuna timu itamtaka.

That's All Folks, muda mwingine!!!!!!!!!

No comments:

Post a Comment