Friday, August 17, 2012

Vermaelen Captain Mpya wa Arsenal, Arteta msaidizi

Arsenal Wenger  amesema kwamba beki wa kati wa Arsenal na nahodha wa Belgium ndiye atakayechukua mikoba ya ukapteni ya mshambuliaji Robin van Persie aliyetimkia Man United na ataanza rasmi pindi Arsenal watapofungua pazia la Premier League siku ya Jumamosi.

EPL, Thomas Vermaelen, Arsenal v Newcastle United
Thomas Vermaelen amechaguliwa kuabadili Robin van Persie kama nahodha wa Arsenal, manager Arsene Wenger amethibitisha.

Van Persie akiwa keshakamilisha taratibu za kujiunga na Manchester United,Arene Wenger alikua tayari na jina la nahodha mpya mbele ya mechi ya ufunguzi dhidi ya Sunderland.

Mikel Arteta amechaguliwa na Wenger kua nahodha msaidizi ikiwa huu ndio msimu wake wa pili klabuni akiwa kasajiliwa kotokea Everton majira ya joto yaliyopita.
"Nahodha mpya sasa ni Vermaelen na [msaidizi wake ni] Arteta," Wenger aliwaambia waandishi wa habari. "Tuna wachezaji wengi wanaoweza kua manahodha katika timu hii."

Vermaelen alijiunga na the Gunners akitokea Ajax June mwaka 2009, na mara moja akajiimarisha na kua maarufu miongoni mwa mashabiki wa klabu yake, akifunga katika mechi yake ya kwanza (debut) dhidi ya Everton na akaendelea kufunga magoli muhimu katika msimu wake wa kwanza.

Baada ya kuwa nje kwa kipindi kirefu kutokana na majeruhi aliyokuwa nayo, nahodha huyo wa Belgium alirudi tena uwanjani zikiwa zimesalia mechi chache msimu kumalizika na alitengeneza ngome thabiti na Mfaransa Laurent Koscielny.

Arsenal watawakaribisha Paka Weusi (jina la utani la Sunderland) siku ya Jumamosi  jioni kwa majira ya Tanzania katika kiwanja cha Emirates wakitaraji kuanza vizuri na kuongeza nguvu ili wapate nafasi zaidi ya watatu waliyofanikiwa kukamata msimu uliopita wa Premier League, na Wenger anajua hiyo mechi itakuwa ngumu kwao.

Alisema: "Kwa kawaida mechi za ufunguzi hua nzito na ngumu sana, utakua mchezo wa maguvu. Tutatakiwa kutengeneza nafasi." alimalizia.

Ramadhan Kareem!!!!!!!!!!



No comments:

Post a Comment