Friday, September 7, 2012

Sagna Achukizwa Na Arsenal Kuuza Mastaa

Arsenal wanaingia tena katika sakata jipya la wachezaji wao kuhoji jinsi timu hiyo inavyoendesha masuala ya kuuza wachezaji muhimu.

Safari hii ni Bacary Sagna, ambaye anaishutumu timu hiyo kwa kuwauza Robin vab Persie na Alex Songi huko yeye mwenyewe akishindwa kuthibitisha kama ataendelea kuwepo klabuni hapo. 

Sagna aliliambia gazeti la L'Equipe: 'Pindi wachezaji wenu wawili bora wanapoondoka, lazima utaanza jiuliza maswali.

'Kuna wakati mashabiki hunifuata na mtaani na kuniuliza, cha ajabu hata mimi mwenyewe sijui.
'Kila mtu alijua RVP angeondoka, lakini sio Song.
'Bado mdogo, ana miaka 24 na akiawa amebakiza miaka mitatu katika mkataba wake. Tumepoteza sana.
'Baada ya msimu huu kumalizika nitabakisha mwaka mmoja.'

Alex Song poses with former Spanish football player Andoni Zubizarreta (L) and Barcelona's deputy sporting director Josep Maria Bertomeu
Haijampendeza Sagna kuona Song anakwenda Barca
 Ingawa ametoa madai hayo, inasemekana Arsene Wenger leo kaamuru yaanze mazungumzo na wawakilishi wa mcheaji huyo juu ya ofa mpya ili akubali kuongezea mkataba na timu hiyo.


Sagna kwa sasa anapokea pauni 60.000-kwa-wiki ila anatarajia kupata nyongeza ya mshahara kama atakubali kusaini mkataba mpya.
Hali hii kama Samir anavyoonekana ndio anayoitaka Sagna, makombe!
Sagna- ambaye hajawahi kupata kombe lolote akiwa Arsenal - aliongeza: ' MImi ndiye mchezaji pekee kwenye kikosi cha kwanza ambaye nimebaki kutokea 2007. Mwezi May, nilikua nikiangalia kwenye tv Manchester City wakipita mitaani kuonesha taji la Premier League na nikawaona Samir na Gael (Clichy) wakiwa wamebeba kombe, nami nataka pia kubeba makombe. 

SIKU NJEMA!!!!!!!!!

No comments:

Post a Comment