Friday, September 7, 2012

Siwezi Hamia Man City - C. Ronaldo

Cristiano Ronaldo ameapa hawezi kamwe kujiunga na manchester City ikiwa Sir Alex Ferguson bado ni Bosi wa manchester United.

Staa huyo aliyenunuliwa na Madrid kwa kitita cha pauni milioni 88, hana raha Bernabeu - na hilo linawatoa udenda Manchester City.

Chanzo cha habari karibu na Ronaldo (27) kilisema: ' Cristiano siku zote yupo karibu na Alex Ferguson na mara kwa mara huwa wanaongea, Cristiano hawezi kufanya kitu cha kumuumiza Ferguson kwa kujiunga na mahasimu wao.'

Kama baba na mwana: Kuna maelewana makubwa kati ya Ronaldo na Sir Alex 

Huvi karibuni Ronaldo alielezea jinsi Sir alex Ferguson alivyomuhimu kwake.
Alisema: 'Nilipojiunga na United nilikua na miaka 18 na Ferguson ni kama baba kwangu. Alinifundisha vitu vingi sana.

'Nimefanya nae kazi kwa miaka sita na ni mtu mzuri sana, kocha mzuri sana. Sir Alex na Mourinho ni ni makocha bora kabisa Duniani.'

Ila Ronaldo kwa sasa hana furaha Real Madrid na anataka mshahara wa pauni  520,000 kwa wiki.

AlhAmisi NjEmA!!!!!!!!!!! 

No comments:

Post a Comment