Sunday, August 12, 2012

Kama Alex Song Hatobadilika, Auzwe Barca

Najua sitowafurahisha mashabiki wa Arsenal ila kwa nionavyo mimi Arsenal wanahitaji Kiungo Mkabaji wa hali ya juu, swali  hapa ni je Song ni kiungo mshambuliaji ama mkabaji?
Alex Song; je hufuata maelekezo ya Arsene Wenger? 
Baadhi ya mashabiki wa Arsenal wanaamini ni Song ni mtaalam anayeweza kufungua beki pinzani na ni kati midfielders bora Ulaya.
Wengine hamuona kama ni mchezaji asiye makini na ulinzi na hukosa nidhamu ya ulinzi na kupenda zaidi kupanda mbele.
Kwa fikra zangu sikuwahi dhani Song angekuja kua mchezaji alivyo sasa. Kamwe sikuweza dhani kama angeweza kufanikiwa akiwa Arsenal. Improvement aliyopata ni ya hali ya juu, pongezi kwake na pia Arsene Wenger. Hata Wenger anakiri anashangazwa na Song alivyokua kimpira kulinganisha na alivyokua.
Song bila shaka ame-improve kwa kiwango cha kustaajabisha, tangu mchezo dhidi ya Fulham mwaka 2006 wakati alipotolewa na Wenger kipindi cha mapumziko kwa kuvurunda na baada ya miezi miwili iliyofuata kupelekwa kwa mkopo Charlton. Kwa wakati ule nilidhani ndio ulikua mwisho wake na asingeweza tena kucheza Premier League.
Alex Song akimkaba Carlos Tevez... je hii inatosha? 
Song sasa ni moja kati ya majina ya kwanza kabisa kwenye list ya Arsene Wenger apangapo timu, tokea kua mchezaji wa hovyo mpaka mchezaji anayezivutia timu kubwa Ulaya, ikiwamo Barcelona . Nionavyo mimi si kama wanamtaka kwa uwezo wake wa ukabaji.
Song anapenda kupanda mbele ni dhahiri, na msimu uliopita ameweza kutoa pasi nyingi zilizozaa magoli matamu na hasa kumtafuta Robin van Persie.
Mfano pasi alizomtolea Van Persie dhidi ya Liverpool na Everton ndizo pasi bora zaidi Premier League msimu uliopita. Amemaliza akiwa wa nne kwa kutoa pasi za kuzaa magoli, nyuma ya David Silva, Antonio Valencia na Juan Mata - na akiwa sawa na Emmanuel Adebayor - kwa assists 11.
Ila kwa mara ya kwanza alipoanza kupata namba ya kudumu Arsenal, haikua kwa uwezo wake wa kushambulia. Ilikua kwa uwezo wake wa kusaidia mabeki wanne wa mwisho(kukaba).
Hili ndilo hasa litakalomfanya Arsene Wenger afikirie mara mbilimbili juu ya kumuuza ama kumbakisha. Barcelona wamekua wakimvizia na wanaweza wakatoa ofa.
Song ana mkataba na Arsenal mpaka 2015. Arsenal hawana ulazima wa kumuuza na hata Song hajadhihirisha kama anataka kuondoka.
Kama akiuzwa, utakua ni uwamuzi wa Arsenal. Na si pande nyingine yoyote.
Na fikra zanijia kwamba Wenger anaweza muuza Song hasa ikiwa atakua na uhakika wa kumnasa Yann M'Vila.

Yann M'Vila: aweza kua mbadala wa Song. 
Arsenal wamemfuatilia kiungo huyu wa Rennes kwa muda mrefu sasa. Ila anajulikana kwa hulka mbovu hasa nje ya uwanja zilizowafanya Arsenal kupunguza mshawasha wa kumtaka kipindi cha majira ya joto. Hata hivyo, kama Song atauzwa basi mshawasha utarudi upya.
Thamani yake ni kati ya paundi za Uingereza milioni 10 mpaka 15, ila kwa vurugu na tabia zake Rennes wanaweza kumuuza hata kwa paundi milioni 10.
Pia sio siri kwamba Arsenal wanamkodolea macho mchezaji wa Real Madrid na kiungo wa Kituruki Nuri Sahin, na watazidisha juhudi hasa kama Song ataondoka hii summer.
Sahin ni hazina hasa, uchezaji wake ni tofauti na Song ila atawaongezea nguvu na machaguo zaidi kwenye nafasi za kiungo ambazo wamekua wakionekana kukosa cover za kuaminika kwa misimu ya hivi karibuni. Wanatakiwa kununua beki mwingne kwani Bacary Sagna atakosa mechi za mwanzo za msimu unaoanza punde.

Picha ya mfano Nuri Sahin akiwa ndani ya uzi wa Arsenal.  

Ila kwa nionavyo mimi, mpaka kufikia September 1(deadline day) Song atakua bado ni mchezaji wa Arsenal. Ila hili si uhakika.
Sawa na, Robin van Persie bado haijaeleweka vizuri. Si haba akaondoka dakika za mwisho ama akawepo.
Mashabiki wa Arsenal kwa mara ya kwanza tokea miaka 7 iliyopita wanamatumaini mepya kupitia manunuzi ya Santi Cazorla, Olivier Giroud na Lukas Podolski na hili litamfanya van Persie afikirie mara mbilimbili.
Santi Cazorla: je atafanya RvP abadili mawazo?

Kwa Manchester United wanaonekana watarudi tena na ofa mpya kwa Arsenal juu ya kumnyakua van Persie . Manchester City na Juventus wameshatoa ofa ambazo zilitupiliwa mbali.
Nadhani hata kama van Persie atauzwa, Arsenal wapo kamili kwa karibia idara zote. Van Persie - wapenzi wa Arsenal wakubali wasikubali - aliwabeba dhahiri kwenye baadhi ya michezo msimu uliopita. Sasa wana machaguo zaidi kwa ushambulizi.
Kama Arsenal wakimuuza Song na kumsajili M'Vila hapo kiulinzi watakua imara zaidi, kwa mawazo yangu. Pia wana Mikel Arteta na Cazorla kwenye kiungo. Jaalia, Jack Wilshere nae arudi mapema.
Ila kila timu inahitaji mhimili. Song ni lazima arudi kua imara na mwenye nidhamu katika msimu huu. Je ana ufundi tosha wa kumfanya kucheza Barcelona? Hilo jibu wewe.
Assists zake ni za kuvutia ila hili si jukumu lake kugawa mipira ya mwisho. Kama hatozingatia kulinda zaidi ya kupanda mbele na kuwaacha mabeki wakiwa wazi kwa counter attacts, basi Arsenal wamuuze na uangaliwe ustaarabu mwingine.

Premier League assists kwa msimu 2011-12

David Silva, Manchester City -15
Antonio Valencia, Manchester United - 13
Juan Mata, Chelsea - 13
Alex Song, Arsenal -11
Emmanuel Adebayor, Tottenham -11
Gareth Bale, Tottenham - 10
Nani, Manchester United -10
Samir Nasri, Manchester City -9
Stephane Sessegnon, Sunderland - 9
Robin van Persie, Arsenal - 9
Sergio Aguero, Manchester City - 8
Ryan Giggs, Manchester United - 8
Theo Walcott, Arsenal - 8
Toa comments zako hapo chini............... Mpaka muda mwigine. Ramadhan Kareem.


No comments:

Post a Comment