Friday, August 17, 2012

Wenger: Song naweza Uza Barca

Meneja wa Arsenal Arsenal Wenger amekubali kwamba Alex Song anaweza kua mchezaji anayefuata kuondoka klabuni hapo msimu huu, Barcelona wakiwa mstari wa mbele kufukuzia saini yake. 

Wenger ambaye kwa kawaida hua si muwazi  kwenye mambo ya kuuza na kununua wachezaji ila safari hii amesema anaweza muuza Song, ikizingatiwa kwa sasa van Persie ni mchezaji rasmi wa Mashetani Wekundu.
Arsenal hawajaamua kumuuza Song ama kumbakisha

Akijibu maswali kuhusu mechi za ufunguzi wa msimu mpya  jumamosi. Wenger alipoulizwa kama Song atakuwepo ama atauzwa alijibu : " Yote yanawezekana, ila akili yangu ipo zaidi kwenye mechi ya ufunguzi na Sunderland. Uamuzi kuhusu Song bado sijaamua."

Alipoulizwa kama kuna ofa wamepokea kutoka Barca alijubu: "Hapana, siwezi kukwambieni zaidi. Wenger alionekana kua wazi kuuza, akisifu wingi wa wachezaji wa kiungo alionao.

"Kiungo ni eneo tofauti kwa sababu tuna viungo tisa ama kumi wa kiwango cha juu," alisema. " Leo tu tuna viungo sita ama saba ambao wako tayari kwa mchezo, ukiongeza Wilshare na Frimpong ambaye yupo mbioni kurudi. Diaby ameshapona, Arteta, Cazorla, Ramsey, Oxlade-Chamberlain naye nimeamua atakua anacheza kiungo wa kati- kwa hiyo kiungo ni eneo ambalo tunaweza kufanya maamuzi yeyote bila kuathirika."

No comments:

Post a Comment