Tuesday, August 14, 2012

Liverpool yamnyakua Joe Allen

Joe Allen: Akithibitisha kujiunga na Liverpool
Liverpool imekamilisha kumsajili kiungo wa kati wa kimataifa Joe Allen wa Wales.
Allen, mwenye umri wa miaka 22 alikamilisha usaili wa kimatibabu siku ya Ijumaa.
Anakuwa wa pili kusajiliwa na meneja wa Liverpool Brendan Rodgers baada mshambuliaji wa kimataifa kutoka Italy Fabio Borini.
''Najisikia vizuri sana. Kila mtu anajua historia ya club hii, ni club kubwa sana, na ninafurahia kujiunga nayo,'' aliiambia wavuti ya club hiyo.
"Mapenzi ya mpira waliyo nayo watu hapa ni kitu ninachoshirikiana nao na ninataka kuwa sehemu yake.
"Nina shauku ya kuwa sehemu ya miaka ijayo ya mafanikio kwa timu ya Liverpool."

Rodgers anaamini Allen atakuwa kiungo muhimu kumuwezesha kuleta mtindo wake wa uchezaji katika timu ya Liverpool.
"Nimefurahi sana sana kwamba Joe amefanya uamuzi wa kuja kujiunga nasi katika safari hii," amesema Rodgers.
"Joe ni mchezaji ambaye uwezo wake unaweza kutumika katika eneo lolote katika timu hii. Uwezo wake wa kutawala na kumiliki mpira ni kitu muhimu katika juhudi zetu za kupata mafanikio uwanjani''.
CHANZO: BBC

No comments:

Post a Comment