Tuesday, August 14, 2012

Jack Rodwell aenda Manchester City

Jack Rodwell kwenye ofisi za Man City

Manchester City imekubali kumsajili Jack Rodwell kutoka Everton kwa kitita kilichowekwa kuwa siri.
Kiungo huyo wa kati wa miaka 21, atafanyiwa usaili wa kimatibabu siku ya Jumapili.
Rodwell, anayepewa thamani ya pauni milioni kumi na tano na Everton, wiki iliyopita alitajwa na Roy Hodgson katika kikosi cha England katika mechi na Italy siku ya Jumatano.
City kwa sasa hawana Gareth Barry kutokana na jeraha la mguu na pia hatma ya Nigel de Jong bado inabakia kuwa na utata.
Meneja wa Manchester City Roberto Mancini amesema: "Tunafikiria Jack Rodwell ni mchezaji mzuri na wa umri mdogo. Atakuwa kiungo wa kati muhimu kwa timu ya Taifa ya England na kwetu pia. Tunahitaji mtu ambaye anataka ushindi, mwenye mbinu nzuri na mchezaji bora kwa muda mrefu ujao."
Siku ya Ijumaa, Mancini alisema hakuwa na furaha kuona Club hiyo ikiwa inasitasita kununua wachezaji wapya msimu huu wa majira ya joto.
Rodwell ndiye mchezaji pekee wa juu kuingia Manchester City msimu huu wa majira ya joto, ingawaje club hiyo inasemekana kuwa na mpango wa kuwahamisha mshambuliaji wa Arsenal Robin van Persie na Daniel Agger wa Liverpool.
Rodwell ataongeza ufanisi katika sehemu ya kati ya City ambayo imedhoofishwa kutokana na kutokuwepo kwa Barry wa England na utata juu ya De Jong kuhusu mkataba mpya.
De Jong mwenye umri wa miaka 27, yuko katika mwaka wa mwisho wa mkataba wake wa sasa na ananyemelewa na Bayern Munich.
Rodwell aliibuka kupitia timu ya vijana ya Everton baada ya kujiunga nayo akiwa na umri wa miaka saba.

CHANZO: BBC

No comments:

Post a Comment