Thursday, August 16, 2012

Chicharito Kutimkia Arsenal?

Ni kweli Hernandez ataondoka ikiwa atakua mshambuliaji chaguo namba 4? 

 Mshambuliaji wa Manchester United Javier Hernandez, inasemekana hajafurahia zoezi zima la usajili wa van Persie.


 Gazeti la Daily Mirror linamuhusisha mshambuliaji huyo kutimkia Arsenal kwani haelewi hatma yake ya kua mshambuliaji chaguo namba nne.


 Hernandez, ambae msimu wake wa pili 2011/2012 ulikua mgumu akiwa kama mshambuliaji chaguo la tatu, inasemekana hajapendezwa na linaloonekana wazi atakosa kabisa nafasi msimu ujao na kwa habari ambazo hazijathibitishwa amemwambia wazi Ferguson anataka kuondoka. 


Wayne Rooney and Robin Van Persie
Be afraid... Rooney na van Persie wataungana kukamilisha foward lina ya Manchester United
 Wiki iliyopita Ferguson alikua ameshavunjika moyo na kuamini hawezi tena kumpata van Persie, huku akilalama Wenger anataka paundi millioni 30 kwa mshambuliaji huyo.

 Arsenal watapata paundi milioni 24 kwa mshambuliaji ambaye kama asingeuzwa basi angeondoka bure baada ya mwaka mmoja, pia Gunners wanaweza kumpata Chicharito kama taarufa ya Daily Mirror ni ya kuaminika. 


Robin atapokea mshahara wa paundi 200,000 kwa miaka minne na kua mchezaji wa pili katika historia ya Man U kupokea mshahara huo mnono.


 Hapo mwanzoni Ferguson alimlaumu Wenger kwa kujaribu kumuuza van Persie kwa klabu zingine na hataki kabisa kuongea na United ingawa ndio chaguo la van Persie. 


 Baada ya majuma ya kukwepana, inasemekana Ferguson aliwasiliana moja kwa moja na Arsene Wenger ili amruhusu van Persie kujiunga na United.


 Wenger alipinga suala hilo ila ilibidi akubali baada ya ofa ya Ferguson kufikia paundi milioni 24 kwa mchezaji mwenye miaka 29 na ambaye angeondoka bure msimu ujao zaidi akiwa na rekodi mbovu ya kuumia. 


 Mashetani wekundu bila shaka watakua na ngome kali ya mashambulizi kwa kuwa na washambuliaji wawili walioongoza kwa ufungaji Premier League ikiwa msimu uliopita kwa pamoja walitikisa nyavu mara 71 kati yao. 


 Je wadhani Chicharito ataondoka? kama sivyo nini hatma yake ikiwa haafiki kua chaguo la nne?

No comments:

Post a Comment