Friday, August 31, 2012

Theo Walcott Kubakia Arsenal Kwa Sasa.


Habari zinasema kwamba kuna uwezekano mkubwa  Theo Walcott akabakia Arsenal majira haya baada ya mazungumzo ya faragha na meneja wa Arsenal Arsene Wenger mapema hivi karibuni.
Inafahamika kuwa kijana huyo ametoa ahadi kwa kauli ingawa hajatia saini mkataba mpya wa kudumu na atatakiwa kufanya hivyo.

Arsenal iliamua kumpa nyongeza kwa kukubali kitita cha pauni za Uingereza cha pauni 75,000 kwa kila wiki kwa kipindi cha miaka mitano ya mkataba lakini akakataa na baada ya hapo imedhihirika kuwa mchezaji huyo pamoja na kuomba mshahara mkubwa anataka abaki kuichezea Arsenal.
Mabadiliko haya yamekuja baada ya kijana Walcott kuzungumza na Meneja wake wakati wa mazowezi kwenye uwanja wa Colney, ambapo Wenger aliridhika na moyo wa kijana kutaka kuendelea kuchezea klabu.
Theo Walcott Alex Oxlade-Chamberlain (L) and Theo Walcott of Arsenal warm-up during a training session at London Colney on February 14, 2012 in St Albans, England.
Ox na Theo wakijifua katika uwanja wa mazoezi wa Arsenal Colney juzi
Awali Arsenal ilikuwa tayari kumuuza mchezaji huyo asipokubalia kutia saini mkataba mpya kabla ya siku ya Ijumaa.
Mchezaji huyo mwenye sifa ya kasi kwenye upande wa kulia wa uwanja ana mda wa mwaka mmoja kwenye mkataba wake na Arsenal.
Tangu aondoke aliyekuwa nahodha msimu uliopita, Robbin Van Persie, Walcot aliyesajiliwa kutoka klabu ya Southampton kwa kitita cha pauni milioni 9.1anaonekana kuwa aliyetetereshwa na kuondoka kwa nahodha huyo.

SIKU NJEMA!!!!!!!!!!

No comments:

Post a Comment