Wednesday, August 29, 2012

Theo 4 Sale! Arsenal Yampa Masaa 48 Kusaini Mkataba Mpya Ama Kuuzwa City au Liverpool

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amempa Theo Walcott masaa 48 kuanzia sasa  kuamua kama atasaini mkataba wa miaka mitano kwa malipo ya pauni 75,000 kwa wiki au kuuzwa.
Walcott mwenye miaka 23, anaweza kuuzwa mapema zaidi hata kabla ya muda wa mwisho wa kufunga usajili Ijumaa hii, huku Manchester City na Liverpool wakiomba kufahamishwa juu ya kinachoendelea tayari kwa kumnyakua. 
On the move: Theo Walcott is locked in negotiations with Arsenal about a new deal - but it looks as though the winger will leave the Emirates
Theo yupo mazungumzoni na Arsenal ila uwezekano wa kubaki ni mdogo  
Ikibidi kumuuza Arsenal watataka kiasi cha pauni milioni 12 kwa kua amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake wa sasa hivyo bei yake kushuka.
Kama Theo akikataa kusaini mkataba - kuna chaguo moja kati ya mawili Arsenal wanatakiwa kuchagua - kumuuza sasa ama kuhatarisha aondoke bure majira ya joto ya usajili yanayofuata. 

Theo Walcott - Queens Park Rangers v Arsenal - Premier League
Theo yupo mazungumzoni na Arsenal ila uwezekano wa kubaki ni mdogo   
FullSoka ilitaarifu jinsi wawakilishi wa Walcott walivyofanya mazungumzo ya kurefusha mkataba Makao Makuu ya Arsenal - Colney HQ ambayo hayakuzaa matunda. 
Walcott yupo ndani ya miezi 12 ya mwisho ya mkataba wake na Arsenal, na bado hajatia saini ili kurefusha mkataba huo, ingawa mazungumzo yanaendelea  inaonekana Walcott hatosaini mkataba huo.

In demand: Liverpool and Manchester City are observing developments
Livepool na City wanasubiria kwa hamu kumnyakua
Kwa mambo yalivyo, kufikia Januari, Walcott anaweza kuanza kufanya mazungumzo na klabu za nje na majira ya joto ya usajili yatakayofuata kuondoka bure.
Liverpool na City wako tayari kumnasa winga huyo iwapo hatotia saini.

Fast-tracked: Serge Gnabry
Serge Gnabry: Mrithi wa nafasi ya Walcott iwapo ataondoka Emirates  
Kama Arsenal wakilazimika kumuuza na kukosa mbadala kabla dirisha la usajili kufungwa, basi mchezaji aliye kwenye akademi Serge Gnabry mwenye miaka 17  ataingizwa kwenye kikosi cha kwanza kuziba nafasi ya Theo.

Wakati huu, Nicklas Bendtner yupo katika maongezi mazito na AC Milan juu ya uhamisho utaogharimu pauni milioni 5 kabla ya dirisha la usajili kufungwa Ijumaa hii.

JUMATANO NJEMA!!!!!!!!!!

No comments:

Post a Comment