Saturday, September 1, 2012

C. Ronaldo - Aina 10 za Ushangiliaji Wake na Anachomaanisha


Christiano Ronaldo amefunga magoli ya kila aina msimu uliopita. Kuna mpenzi wa FullSoka ametaka nimuelezee aina fulani ya ushangiliaji wa Ronaldo, hapa nitatumia fursa hii kuelezea aina 10 maarufu za ushangiliaji wake.

"The Silencer"
1. "The Silencer" huweka kidole cha shahada  katikati ya mdomo wake: huu huwa ni ujumbe kwa mashabiki wa timu pinzani na humaanisha sasa wanyamaze baada ya kuwa wameishangilia sana timu yao ama waliokuwa wanambeza. 

Mfano ni mechi ngumu kati ya Real na Atletico Madrid kombe la Copa Del Rey robo fainali ya pili baada ya kufunga bao la ushindi.


"The Thumb Sucker"
2. "The Thumb Sucker" huweka kidole gumba chake kimywani huku akikinyonya. Hua ni ishara kwa mwanawe wa kiume aliye na umri chini ya mwaka mmoja aitwaye Christiano Ronaldo "Junior".
"The Claw" 
3. "The Claw" ishara ya makucha yaliyotayari kushambulia au ishara ya kupanda kuelekea juu. Hii hua ni ishara kwa mwanae(CR Junior) na girlfriend wake(Irina Shayk): pindi anapokua na mtoto wake ishara hii ndiyo humfanya mtoto huyo afurahi hata kama alikua analia.

Aliigundua pale alipomuiga mtoto wake huyo baada ya kumuona akijaribu bila mafanikio kuparamia kingo za kitanda chake cha kitoto ili atoke. 

Naye alipomuiga kwa kuonesha ishara ya "The Claw" mtoto ikawa kicheko, basi tokea hapo naye imekua ni ishara kuu kila anapofunga goli.

             
Akimuonesha "The Claw" girlfriend wake Irina anayeonekana kaboreka Barnebeu, labda akidhani nae atacheka kama mwanaye, ni siku Real Ilipoifunga Vallecano 6-1 ye akifunga Hat-Trick Ronaldo akijinyonganyoka wala huwezi kuita kucheza mziki 
4. "The Dance" Hunyoosha mikono mbele huku akijinyonganyonga na kurukuruka. Kama jina lenyewe lilivyo "kucheza mziki", hii ishara hua ni kwa wachezaji wenzake, aliifanya mara moja tu nadhani baada ya kugundua ye si mchezaji mzuri wa muziki basi hata hakuirudia tena."The Fist Anger" 
5. "The Fist Anger" Hukunja ngumi mikono yote miwili kisha huku akipiga mayowe hunyanyua mkono wa kulia huku akiwa kakaza mwili. Hii hua ni ishara kwa mashabiki, na wachezaji wenzake hasa anapofunga baada ya mchezo kua mgumu. Ishara hii huonesha uwezo, nguvu na hasira. Picha hii ilichukuliwa kati ya mchezo dhidi ya Rancing Santander uliopigwa Santiago Bernabeu.


"The Deaf" 
6. "The deaf" - Christiano Ronaldo hua anatukanwa sana katika viwanja vingi vya ugenini hasa Nou Camp. Ushangiliaji wa kuweka kiganja kilichofunguka nyuma ya sikio hua ni kwa mashabiki pinzani, tofauti na "The Silencer" ambayo huwataka wafunge midomo hii hua anaashiria hajasikia matusi yao kwa ishara kwamba wazidishe sauti.

"The Sliding Machine" 
7. "The Sliding Machine" Ishara ya mambo kuwa rahisi na  kufurahia mchezo hasa anapofunga magoli mengi. Urahisi huo huufananisha na kuteleza kwenye zile tube za kuchezea watoto (Aqua Splash). 

"From Ronaldo To Ronaldo"

8. "From Ronaldo To Ronaldo"  Ishara ya kushika kichwa na kuvuta kumbukumbu ya jambo flani. Hii anaashiria kumtunuku Ronaldo De Lima na kukumbusha ukubwa wa jina "Ronaldo", Ronaldo De Lima ndiye hasa aliyeanzisha ushangiliaji huu akiwa pia Real ila akimaanisha kitu tofauti. Kwa CR7 hufanya hivyo kuashiria ukubwa wa jina lao hilo -Ronaldo- 

"The Kindergatten"  
9."The Kindergatten" Baada ya kufunga humvuta mkono mchezaji mwenzake aliyempa pasi ya goli kwa mfano wa kumuongoza njia ama kumsaidia kuvuka barabara mtoto wa chekechea. Picha hii ni pale alipofanya na DiMaria kwenye mashindano ya UEFA Champions League, dhidi ya Ajax.

"The Claw Mirror"   
10. "The Claw Morror" - Christiano hurudia ishara ya "The Claw" ila mara hii hufanya kwa msaada wa mchezaji mwenza huku wakiwa wanaangaliana. Hii ilikua mechi dhidi ya Getafe. Kama maana ya kwanza ni kuonesha furaha na kumshirikisha mwenza wake kwenye furaha yake.


 Ok, sasa wajua hua anamaanisha nini...................ukiwa na swali tuma kwenye email iliyopo hapo juu (fullsoka@gmail.com) nasi tutajibu bila kuchelewa.

Kazi Njema!!!!!!!!!

No comments:

Post a Comment