Friday, August 31, 2012

Man U Wamkosa Dembele Dakika za Mwisho, Atua Tottenham

Jana usiku klabu ya Manchester United walimkosa kiungo aliyekuwa akichezea klabu ya Fulham ambaye amesajiliwa na timu ya Tottenham Hotspurs.
Dembele ambaye hua akiwasumbua Mashetani Wekundu kila mara anapokutana nao uwanjani, alikuwa akitakiwa na Alex Ferguson ila Tottenham walilipa zaidi na wakati Mzee Ferguson akifikiria kuongeza dau, tayari Spurs walikuwa wamesha kamilisha usajili huo.


Dembele alin'gara dhidi United katika mechi iliyochezwa Old Trafford hivi karibuni 
Gazeti la Guardian leo liliripoti Man U wanamfukuzia mchezaji huyo, lakini Tottenham waliokuwa na dhamira zaidi na mchezaji wa kiungo baada ya kiungo wao wa kutegemewa Luka Modric kutimkia Real Madrid mapema wiki hii.

Moussa Dembele aliyetua Spurs kwa kikita cha pauni milioni 15, anakuwa ni mchezaji wa pili kwa Manchester United kumkosa baada ya Lucas Moura naye kubadili mawazo na kuchagua kutia saini PSG ya Ufaransa.

IJUMAA NJEMA!!!!!!!!!!!

No comments:

Post a Comment