Friday, August 31, 2012

Berbatov Ajiunga Fulham, Apunguza Mshahara, Azikataa Juventus na Fiorentina

Dimitar Berbatov jana amekubali kujiunga na timu ya Fulham na atapokea mshahara mdogo kulinganishwa na ule ambao angeupata kama angekwenda Juventus ama Fiorentina zilizokuwa zikimuwinda.

M-Bulgaria huyo amekubali kulipwa pauni 50,000 kwa wiki huku akiingia mkataba wa kuichezea klabu hiyo kwa miaka miwili.

Mchezaji huyo anarudi tena katika jiji la London baada ya mwaka 2008 kununuliwa na Manchester United kwa ada ya pauni milioni 30.7 akitokea klabu nyingine ya London Tottenham.

Moussa Dembele
Fulham wamemuuza Dembele kwa Spurs pesa zilizosaidia kufanya usajili
Kishawishi kikubwa kwa Berbatov kujiunga na Fulham ni kocha wa sasa wa Fulham Martin Jol amabye ndiye aliyemnunua Berbatov mwaka 2006 kutokea Ujerumani kujiunga na Tottenham. 
Hii itaipa nguvu Fulham walioondokewa na kiungo wake mahiri Moussa Dembele jana na kutokuwa na uhakika wa kubaki Clint Dempsey.

IJUMA NJEMA!!!!!!!!!

No comments:

Post a Comment