Saturday, September 1, 2012

Mancini Avunja Rekodi ya Usajili Mwaka Huu, Alalamika Hajaridhika!

Roberto Mancini amekuwa mwenye kulalamika juu ya usajili ulivyokwenda kwenye klabu yake ya Mancester City licha ya kutumia pauni milioni 52 kwa kununua wachezaji wapya watano katika majira haya ya usajili.


City wamewasajili Javi Garcia pauni milioni 16, Matija Nastasic pauni milioni 12, Scott Sinclair pauni milioni 6, Maicon kwa pauni milioni 3 na Jack Rodwell aliyemnunua mapema kwa pauni milioni 15.

Mancini alilalamika City wameshindwa kupata wachezaji chaguo la kwanza aliokuwa akiwataka yeye - akiwakosa Robin van Persie, Eden Hazard, Javi Martinez na Daniel De Rossi.

Alilalama: " NI vigumu kufanya kila kitu katika wiki moja ama siku kumi.
"Ligi ilipokwisha nilikaa na Bodi. Tuliongelea kuhusu wachezaji niliowataka ila mara nyingine ni vigumu kupata wachezaji wote unaowataka.
Unabidi uwe na chaguo mbadlala Ila kwa wachezaji tuliowapata, nimefurahi"


Mancini akiwa na winga mpya aliyemnunua Scott Sinclair kutoka Swansea
Mancini alitumia muda mwingi wa kipindi cha usajili kumlaumu Brian Marwood Mtawala wa Soka City kuhusu kutojishughulisha na kuwanunua wachezaji aliowapendekeza.

Waliowakosa:mchezaji kutoka Arsenal van Persie alikwenda Man U kwa pauni milioni 24, Hazard akijiunga na Chelsea kwa pauni milioni 32, Martinez akaelekea Bayern Munich kwa pauni milioni 32 pia na De Rossi akibakia Roma.

Ameambulia mlinzi wa kati Nastasic(19) akiitwa 'Nemaja Vidic Mpya'  kutokea Fiorentina, winga Sinclair (23) akitokea Swansea, M-brazili Maicon(31) kutokea Inter Milan.

Na kiungo mkabaji, Garcia (25) muda mfupi kabla dirisha la usajili kufungwa, atachukua nafasi ya Nigel de Jong aliyeuzwa AC Milan kwa dau la pauni milioni 5.

WIKIENDI NJEMAAA!!!!!!!!!

No comments:

Post a Comment