Saturday, September 8, 2012

Kuondoka Ama Kubaki United, Mimi Sie Muamuzi - Wayne Rooney

Wayne Rooney amekubali kwamba mwenye maamuzi juu ya yeye kubakia United ama kuondoka si yeye.

Tokea kuwasili kwa mshambuliaji mwingine klabuni hapo Robin van Persie na Ferguson kua anamuanzisha benchi, ni dalili ya wazi hadhi yake klabuni hapo ipo hatarini.

Wayne Rooney
Mahusiano kati ya Fergie na Roo si mazuri

Kuwepo kwa Danny Welbeck, Javier Hernandez na straika mpya Angelo Henriquez, Ferguson hawezi tena kuletewa maringo na Rooney kwa kua ana wachezaji mbadala kwa nafasi ya ushambuliaji.

 Rooney alisema; ' Mara zote nimekua nikisema kama nitaendelea kuhitajika hapa basi nitaendelea kuwa mchezaji wa Manchester United.'


Akikumbushia uamuzi wake wa kusema hadharani kwamba anataka kuondoka, 
Rooney alisema 'Ni dhahiri miaka michache iliyopita kulikua na jambo, ila nilijishukia na haraka nilisema nilifanya makosa.

'Ikiwa watu wanataka niendelee kua mchezaji wa Manchester United, hilo ndilo nitakalo kua.'Kuja kwa Robin kuna maanisha Wayne si tena mshambulizji namba moja


Ferguson hafurahishwi na Rooney kuonekana kunenepa na kua mzito mwanzoni mwa msimu huu, na mahusiano ya wawili hao bado si mazuri tokea malumbano ya mchezaji huyo kutaka kuondoka na tabia zake kwa ujumla.

Hayo yanaweza pelekea Rooney kuondoka United, hasa ukizingatia Sir Alex hamtegemei sana kwa sasa.

Tokea Rooney anajiunga na Man U mwaka 2004, amekua na namba ya kudumu katika kikosi cha Sir Alex, ila kwa sasa kama atabaki basi itabidi azoee kuanzia bechi mara zingine ama ajenge maelewana mazuri uwanjani na van Persie ili ajihakikishie nafasi.

 'Huwezi fikiria tu utacheza,' alisema Rooney. ' Ila mara zote nimekua nikijituma sana kuhakikisha Bosi anachezesha.

'Nimepata jeraha hili ila najituma sana gym kuhakikisha kwamba wakati nitakapoambiwa niko poa kurudi kiwanjani, narudi uwanjani na kufunga magoli.

'Ni jambo zuri kwa meneja, na sisi tunatakiwa kuhakikisha tuna muumiza kichwa.
'Napanga kurudi kwenye timu na kujaribu kutengeneza maelewano kiwanjani na Robin.

'Tokea nilipojiunga na United nimekua na maelewano mazuri na kina Ruud van Nistelrooy, Louis Saha, Carlos Tevez, Dimiter Berbatov, Javier Hernandez na Danny Welbeck.

'Kwa washambuliaji wa sasa inanibidi kuendana na hali. Kama nikicheza nyuma yao ama kama mshambuliaji wa mwisho. Mara zote hua naweza na kufiti vizuri.' Rooney alitanabaisha.


Wayne Rooney of Everton celebrates scoring the equalising goal during the FA Barclaycard Premiership match between Arsenal and Everton
Enzi hizo: Roo anakubali mambo yamekua ni kupanda na kushuka tokea alivyoanzia Everton
JUMAMOSI NJEMA KWA WANA PREMIER LEAGUE WOOOOOOOTE!!!!!

No comments:

Post a Comment