Tuesday, September 4, 2012

Arsenal Sasa ni Bora Kuliko Alipokuwepo van Persie - Wenger

Arsene Wenger anaamini wachezaji wake wa sasa wanaweza kufanya makubwa zaidi ya aliyoyafanya Robin van Persie Arsenal.


Hilo limekuja baada ya kuondoka kwa nahodha na mfungaji bora wa ligi msimu uliopita kujiunga na United mwezi jana ulileta wasiwasi Emirates, na Arsenal kuichakaza Liverpool katika uwanja wake wa nyumbani Anfield jana jioni.

Wenger amefanya mabadiliko katika kikosi na alisema: "Sisi ni bora kuliko msimu uliopita? ni mapema kusema hivyo lakini hilo ndilo lililopo.

"Kuna vitu vidogo vidogo vya kushughulikia na dalili zinaonesha mambo ni mazuri. Angalia viungo wetu. Tuna Arteta, Cazorla, Wilshere, Coquelin, Rosicky, Ramsey.


Vermanator: Nahodha wa Arsenal mzoezini kabla ya meechi dhidi ya Liverpool jana 
Wenger aliongeza: "Kuna kupigania nafasi na ubora upo pia. Tumecheza mechi mbili za mwazo ingawa hatukufanya vema sana lakini unaona dalili za mambo mazuri, labda tulikosa kichocheo.

"Tulimaliza mpira tukijihisi tulifanya vema"

Wachezaji wapya wa wanaompa matumaini Wenger
katika mechi dhidi ya Liverpool Mspanishi Cazorla alivutia sana na Abou Diaby alikuwa kila mahali kwenye kiungo.

Wenger alimalizia: "Kila mtu alifahamu Cazorla asingechukua miezi sita kuzoea na Diaby ni muhimu sana kwetu."

SHUKRANI

No comments:

Post a Comment