Friday, September 7, 2012

Uroho Wa Mshahara Mkubwa Wazuia Nani Kuuzwa Leo

Louis Nani ameendelea kujiweka njia panda na asijue hatma yake, baada ya jana kushindwa kuafikiana na Zenit St. Petersburg juu ya kiwango cha mshahara anachotakiwa kulipwa, hivyo ataendela kuwepo Old Trafford msimu huu. 

Rusia usajili wao ulifungwa rasmi jana saa sita usiku kwa masaa ya Ulaya, hivyo kulikua bado na uwezekano wa Nani kuondoka Man U ingawa dirisha la Usajili lilikua limeshafungwa Uingereza na sehemu nyingi za Ulaya.


Nani ambaye alikua ameruhusiwa kuondoka Manchester United, hataondoka tena kwa sababu ya mshahara mkubwa aliokuwa anataka awe analipwa na klabu hiyo. 

Nani ambaye pia bado hajakubali mshahara mpya aliotengewa na Mashetani Wekundu kama ataamua kubaki, yuko njia panda  Old Trafford kwani si tu amegomewa kukubaliwa kua analipwa pauni 130,000 kwa wiki bali hata uhakika wa nafasi kiwanjani hana.

Nani na GF wake wakiwa katika hafla kuchangia Unicef iliyoandaliwa na United 

Valencia na Ashley Young wanapewa kipaumbele kwa nafasi ya wingi, na kuja kwa van Persie na mchawi Shinji Kagawa kutafanya nafasi yake kuwa finyu zaidi.

Watu wa karibu yake wanasema kwamba Nani anajiona hathaminiwi United kama wachezai wengine. 

Aliondolewa kikosini baada ya United kupata kipigo katika mechi ya ufunguzi dhidi ya Everton na tokea wakati huo hana uhakika wa namba.


New boy: Shinji Kagawa is getting more game-time than Nani
Kagawa anapata nafasi zaidi kulika Nani

Mechi ya Jumapili dhidi ya Southampton aliingia zikiwa zimebakia dakika 29 akipishwa na Kagawa katika ushindi wa 3-2 ni mechi yake ya pili msimu huu, ikiwa haanzi ama akianza lazima atolewe.

ALHAMISI NJEMA!!!!!!!!!!!!

No comments:

Post a Comment