Tuesday, September 4, 2012

C. Ronaldo Adai Hana Raha Madrid Anataka Kuondoka, Chelsea, PSG, Man U na Man City Wajitayarisha Kunyakua

 Crictiano Ronaldo ameziweka klabu za Manchester City, United, PSG, Chelsea katika hali ya kujitayarisha kuingia vitani ili kumpata baada ya kuthibtisha anataka kuondoka Real Madrid.

Mtu wa karibu yake alipoulizwa alisema: "Kweli, Cristiano amemwambia Raisi Florentino Perez anataka kuondoka klabuni hapa."
  

Hayo yamekuja baada ya Ronaldo,27, kufunga goli mbili siku ya Jumapili lakini hakushangilia goli lolote katika hayo mawili dhidi ya Granada. 

Na alipulizwa baada ya mechi alisema: "Nina huzuni na viongozi wa klabu wanajua.
"Ni mambo ya kitaaluma (Professional Issue). Siwezi sema zaidi ya hapo."

Cheer up! Cristiano Ronaldo (pictured arriving at training on Monday) has said he is 'unhappy' with the current situation at Real Madrid
Ronaldo akiwasili kwenye kambi ya mazoezi ya Real jana Jumatatu
Ronaldo ana kifungu katika mkataba wake(release clause) ambacho kinamruhusu kuondoka klabuni hapo kama timu itaweza kuilipa Real pauni milioni 100 (Real wanadai ni zaidi ya pauni milioni 700) na kuweza kumlipa mshahara utakaoanzia pauni 25,000 na kuendelea kwa wiki.

Kwa wakati huu kuna timu chache ambazo zinaweza kufanya hivyo: Manchester City au PSG, na hata Chelsea.

Jose Mourinho pia hatarajiwi kuwepo Real muda mrefu ujao, kuna uwezekano akaondoka majira ya joto yajayo na atapendelea kuondoka na Ronaldo kama ataenda timu zenye fedha za kumwaga kama City au PSG.

Cheer up! Cristiano Ronaldo (pictured arriving at training on Monday) has said he is 'unhappy' with the current situation at Real Madrid
Akisindikizwa kama ilivyo ada kwa wachezaji wote wanapowasili mazoezini
Cristiano alinunuliwa kutoka Manchester United mwaka 2009 kwa ada ya pauni milioni 80, akiwaongoza Real vema kuchukua vikombe msimu uliopita akifunga mabao 46 katika michezo 38 ya La Liga na jumla ya mabao 60 katika mashindano yote aliyoichezea Real - kitu kinachomfanya afikirie labda anatakiwa kuongezewa mshahara.

Ameshaifungia Real Madrid jumla ya magoli 150 akiwa na wastani wa goli zaidi ya moja kwa mechi lakini kwa Spain, Messi ndiye anayeonekana bora. 

Kuna wanasema kitendo cha Messi kuonekana ni bora zaidi yake huwa kinamnyong'onyesha sana.  

Is that it? Ronaldo failed to show much enthusiasm as he bagged two goals in the game
Hichi ndicho alichoweza kufanya baada ya kushindwa kushangilia goli la pili kwa kua hana furaha kuwepo Madrid
Katika mechi ya Portugal dhidi ya Denmark Euro 2012, alipokuwa akikosea mashabiki wa Denmark walikua wakishangilia kwa wakiimba jina la Messi.

Ronaldo hathaminiwi kama ambavyo Messi anavyotukuzwa Barcelona na kituo kimoja cha radio kiliripoti kwamba Ronaldo amemuambia Raisi wa Real kwamba hata katika vyumba vya kubadilishia nguo (Dressing Room) Real Madrid hathaminiki.

Unhappy chappy: Ronaldo said he was 'sad' but refused to elaborate on the reasons why
Akihudumiwa baada ya kujeruhiwa katika mechi dhidi ya Granada
Kama hii itakuwa ni mbinu ya Ronaldo ya kutaka kuongezewa mshahara zaidi, basi inaweza lipa ama ikaharibu kila kitu. Na Real wanaweza kumpa mkataba mnono autakao ila waendelee kujaribu kuwapiku Barcelona, ila kama tatizo la Ronaldo ni furaha, pesa haziwezi kumpa furaha mpaka siku atakayoondoka.

KAZI NJEMA!!!!!!!.

No comments:

Post a Comment