Tuesday, September 4, 2012

Simuheshimu Tena Ferguson - Berbatov

Dimitar Berbatov jana usiku alimshutumu vikali Alex Ferguson na kusema kwamba: " Simuheshimu tena."

Berba alimshambulia Fergie kwa kumpuuza kwa miazi 18 ya mwisho aliyokuwa United.
M-bulgaria huyo alihama Old Trafford na kujiunga na Fulham kwa pauni milioni 4 siku ya mwisho ya usajili.



Alifoka: " Nimehuzunishwa sana na Ferguson. Ila simuheshimu tena kwa sababu ya aliyonitendea."

Berabtov, 31, alinunuliwa na Ferguson akitokea Tottenham kwa ada ya pauni milioni 30 mwaka 2008.

Alikuwa mfungaji bora (akifunga magoli 20) wakati Manchester United wakitwaa taji la Premier League mwaka 2011 - Ila Fergie alimuondoa katika kikosi cha fainali ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Barcelona.

Kichwa chini: Mahusiano kati ya Ferguson na Berbatov hayakuwa mazuri

Berba aliongeza: "Najivunia mafanikio yangu ila nimehuzunishwa na Ferguson kama binadamu. Sidhani kama ananifikiria vizuri kwa sasa.

"Na nilikuwa radhi kusaini mkataba wa kukaa United milele"


Berba alisema: "najisikia vibaya kwa yote yaliyonitokea Manchester. Sikustahili. Ila kocha ndiye mwenye maamuzi.

"Aliniambia anabadilisha mfumo wa uchezaji na sitakuwa tena na mchango.

"Sina cha kuona aibu baada ya mambo kwenda nisivyovyotarajia. Nastahili sifa, nimeshinda makombe, na nimekuwa mfungaji bora.

"Nilipoondoka niliwaaga watu wengi ambao walistahili kuagwa, si wote kwa sababu sikuweza kuwaona wote. Sikuwa nikiongea na Ferguson, na sikutaka kumuaaga."


Berbatov akijaza mafuta katika jiji la London hivi karibuni


Berbatov alikutana zaidi ya mara 10 Ferguson kutaka kujua hatma yake kama anahitajika klabuni hapo. Na mara zote alikuwa anaambiwa yeye ni muhimu hivyo hatakiwi kuhama.

Mchezaji huyo wa zamani wa Tottenham aliambiwa agombee nafasi yake, cha ajabu hata hiyo nafasi ya kugombea hakuwa akipewa.


Aliamua kutaka kuhama klabu baada ya kutemwa kwenye fainali ya klabu bingwa ulaya ila alibadili msimamo wake baaada ya Ferguson kumuomba asiondoke na apiganie nafasi.

Na alipotaka kujua sababu ya kuondolewa kikosini kwenye fainali ya klabu bingwa ulaya - hakupata jibu lililo wazi.

Berbatov alisema: " Sikustahili kuondolewa kwenye kikosi cha fainali dhidi ya Barcelona. Nadhani nilifanya makosa kutokuhama United baada ya mechi ile.

"Niliongea na Ferguson zaidi ya mara 10 ama 15. Nilimuuliza: "Bosi, bada unanihitaji?'
"Alijibu yupo na mimi. Sikuweza kurudi kumuuliza tena kwa kuwa angeweza kunitukana.

SIKU NJEMAAAAAAA!!!

No comments:

Post a Comment