Wednesday, September 5, 2012

Fowardline Ya Rooney na van Persie Itakuwa Balaa Ulaya - Sir Ferguson

Alex Ferguson anaamini ndoto yake ya kupata tena ngome kali ya mshambulizi kama aliyokuwa nayo mwaka 1999 iko mbioni kutimia.

Hilo linatokana na makali aliyoyaonesha Robin van Persie tokea ajiunge na Mashetani Wekundu na matarajio ya kurudi uwanjani kwa Rooney ambaye kwa sasa ni majeruhi.


Ferguson anawafananisha RVP na Roo kama walivyokuwa Driwght Yorke na Andy Cole kwa jinsi walivyokuwa wanatisha miaka 13 iliyopita.

Sir Alex alisema: "Van Persie ni mchezaji anayeweza kucheza nafasi tofauti tofauti.
"Hua hatulii sehemu moja, ni chuo mbadala kwa sehemu tutakayokuwa pungufu kimashambulizi. 

"Rooney yeye anaweza cheza nyuma ya mshambuliaji wa mwisho ama mbele kabisa.

"Hernandez ni mchezaji wa nafasi moja na nafasi hiyo ni mshambuliaji wa mwisho kabisa.

"Je Wayne na Robin wanaweza cheza pamoja? Ndio, hakuna ubishi juu  ya hilo.

"Na Welbeck anaweza cheza nao wote, hakuna wasiwasi juu ya hilo pia."

Sir Fergie anafananisha kikosi cha washambuliaji alicho nacho sasa na cha kile cha mwaka 1999 kilichochukuwa mataji matatu makubwa katika msimu mmoja
Ferguson anasema ngome ya mashambulizi aliyonayo sasa inampa urahisi sana wa kubadili timu. Ni rahisi pia kua bila Roo kwa takribani mwezi baada ya kuchanika paja katika mchezo dhidi ya Fulham wiki iliyopita.

Lakini anakubali kwamba washambuliaji wake wa sasa wanamuweka njia panda kupanga timu kwa ujumla.


Alipoulizwa kama hichi ndio kipindi kigumu katika muda wote aliowahi kufundisha katika kufanya uchaguzi wa washambuliaji, Fergie alijibu: " Kwa washambuliaji, ni kweli kabisa. Ni ngumu zaidi ya mwaka 1999.


"Wakati ule, Dright Yorke na Andy Cole walikua na ushirikiano wa ajabu - kwa hiyo mara zote walikuwa chaguo langu la kwanza. "Ila sasa nina washambuliaji wanaonipa ugumu wa kuchagua moja kwa moja, ndipo ugumu ulipo.Robin van Persie: Sasa ni zaidi ya lulu Old Trafford


FullSoka ilibainisha wiki iliyopita juu ya wasiwasi kama Rooney ataendelea kuwepo Old Trafford kwa kipindi kirefu kinachokuja.

Ni dhahiri hata Rooney atakapopona hana uhakika wa kuingia  moja kwa moja uwanjani kama ilivyokuwa awali.

Na Ferguson anaona hilo linaweza kumuathiri Roo kama ataachwa nje ya wachezaji 11 wanaoanza mchezo, kama ilivyokuwa katika mchezo dhidi ya Fulham, pindi atakapokua fiti.

Alisema: " Itamuathiri. Wachezaji hupenda kucheza kila wiki. Ila kwa sasa hilo si tatizo."

JUMATANO NJEMA!!!!!!!!!!!

No comments:

Post a Comment