Sunday, September 2, 2012

Essien Ajiunga Real Madrid - Mourinho ni Baba Yangu

Michael Essien anatarajia kuwa na mahusiano mazuri na Mourihno kama ya baba na mwana kama waliyokuwa nayo walipokuwa wote Chelsea baada ya kukamilisha usajili wa mkopo Real Madrid.

Tayari Essien amejumuishwa akatika kikosi cha wachezaji 20 kwa mechi ijayo itakayopigwa Bernabeu dhidi ya Granada.

Essien alinyakuliwa na Real kwa mkopo wa muda mrefu kutoka Chelsea dakika za mwisho kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili, Mafahari hao wa Spaini wamemruhusu Lassana Diarra kujiunga na klabu ya Russia Anzhi Makhachkala kwa msimu huu kupisha nafasi kwa Essien.Kujiunga kwake Bernabeu, Essien mwenye umri wa miaka 29 atakutana tena na bosi wake wa zamani, Mourihno ndiye aliyemleta Uingereza mwaka 2005,  na Mghana huyo hafichi furaha yake kuwa tena karibu na mtu anayemuona kama baba yake.

"Hua namuita hivyo (daddy) kwa sababu namuona kama baba. Alininunua Chelsea na tukawa na mahusiano mazuri. Huwa namuelewa sana." alisema Essien ambaye alifaulu vipimo vya afya kabla ya kutia saini mkataba Bernabeu.

"NIlikuwa chumbani kwangu hotelini jana na nikapata simu kutoka kwa 'baba' na alisema angependa kuwa nami hapa"
"Mambo yamekwenda haraka sana ila nimefurahi" 

Akiwa Chelsea amecheza mechi 247 akifunga magoli 25 na mara mbili akishindwa taji la kufunga goli zuri la msimu klabuni kwake.

Real deal: Michael Essien poses after being unveiled by the Spanish giants
Michael Essien akiwa amepozi na jezi atakayokuwa anavaa
Miaka ya hivi karibuni Essien amepata majeraha ila amesisitiza yuko fiti sasa na yuko tayari kufanya mambo Real, "nimefanya mechi za maandalizi na Chelsea na niko tayari kucheza.

"NIlikuwa majeruhi ila ni mambo yaliyopita. Niko fiti  na mwenye nguvu. Kam si hivyo Real wasingenisajili. Wakitaka nicheze hata kesho naweza cheza.

" Baba (Mourihno) ananijua vilivyo, anajua naweza cheza nafasi yoyote atakayotaka nicheze, ukiondoa goli kipa."
Hard-men: Essien talking to Pepe
Essien akiongea na Pepe pamoja na Benzema mazoezini jana 
Kuhusiana na nini kitafuata baada ya muda wa mkopo wake kuisha alisema: " Kwa muda huu nipo hapa kwa mkopo, nitafanya kazi kwa bidii hapa Real Madrid. Na mwisho wa msimu ndio tutaona mambo yamekaaje."

Essien atakutana pia na Luka Modric aliyejiunga na Real Madrid siku ya Jumatatu kutokea Tottenham.

JUMAPILI NJEMA!!!!!!!!!!

No comments:

Post a Comment