Wednesday, September 12, 2012

Wanasoka Wanaoingiza Pesa Nyingi Zaidi 2012 – Wanasoka Matajiri Duniani

Mwanasoka wa Kimataifa wa Argentina, Lionel Messi ndiye mchezaji anayelipwa zaidi duniani kwa mwaka 2012, akifuatiwa na David Beckham wa Uingereza na Mportugal Cristiano Ronaldo akishika namba tatu, hizi nia takwimu za Gazeti la France Football. 

Nyota wa Barcelona, Messi hutia kibindoni euro 33 million (sawa na dola 43.5 million) kwa mwaka, kati ya hizo euro 10.5 million ni mshahara alipwao Nou Camp, euro 1.5 million kama bonus za michezo Barca na euro 21 million  katika matangazo ya biashara na mikataba mingine.


1. Lionel Messi


2012 Mapato: €33 Million ( pauni 27.5m)
2011 Mapato: €31 Million
Utajiri Jumla: $110 Million – (makadirio)
Klabu Ya Sasa: FC Barcelona
Nyota huyo wa Barcelona hujiingizia euro 33 million kutokana na udhamini kutoka kwa Adidas na Pepsi.

2. David Beckham


2012 Mapato: €31.5 Million (pauni 26.2milioni)
2011 Mapato: €19 million
Utajiri Jumla: £160 Million or $260m – kufikia May 2012, imetolea the Sunday Times UK Rich List
Klabu Ya Sasa: Los Angeles Galaxy

Becks, 36, amejikusanyia euro 31.5 million na ameendelea kua maarufu licha ya kucheza Amerika timu ya LA Galaxy.
Mkataba wake na Adidas ndio mkubwa kuliko yote katika tasnia ya michezo, na mingine kama ile ya ObyO watengeneza nguo za ndani huzidi kutunisha mapato yake.
Mwezi May 2011 alisaini mkataba na Samsung kua Balozi wa Kampuni hiyo katika soka.

3. Cristiano Ronaldo


2012  Mapato : €29.2 Million ( pauni 24.3milioni)
2011  Mapato : €27.5 million
Utajiri Jumla: $160 Million – (makadirio)
Klabu Ya Sasa:Real Madrid

Nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo ni namba tatu na €29.2m ingawa ndiye aliyeongoza kwa kufunga La Liga msimu huu.
Ndiye mwanamichezo anayeongoza kua na mafans wengi katika mitandao ya kijamii. Akiwa na fans milioni 26 Facebook, mara mbili ya ya anayemfuatia na wafuasi milioni 3 twitter; ikiwa ni moja ya vizutio kwa wadhamini kama Nike, Armani, Coca-Cola na Castrol.

4. Samuel Eto’o


2012  Mapato:€23.3 Million (pauni 19.4milioni)
2011  Mapato: €13 Million
Utajiri Jumla: $50 Million – (estimated)
Klabu Ya Sasa: FC Anzhi Makhachkala

Katika miezi 12 iliyopita, M-Cameroon ameongeza Puma na Ford kama wadhamini wake. NI mshindi mara mbili wa kombe la Klabu Bingwa Ulaya akiwa Barcelona na Inter Milan.
Ndiye mwafrika mwenye mafanikio kuliko wote waliopata kutokea; ameshinda Mwanasoka Bora wa Afrika mara nne mambayo ni rekodi; mwaka 2003, 2004, 2005 na 2010.

Mshambuliaji huyu wa zamani wa  Inter Milan alijiunga na klabu ya soka ya nchinin Rssian FC Anzhi Makhachkala kwa mkataba wa miaka mitatu na mshahara wa uero 20.5 million kwa mwaka ama kwa maneno mengine dola 28.8 million kwa exchange rates za sasa.

Mkataba na klabu hiyo ya Russia imemfanya kua mwanasoka anayelipwa zaidi katika historia ya soka duniani kama kipengele cha mshahara pekee kikizingatiwa.

Akimzidi C. Ronaldo kwa euro 13 million ( pauni 19milioni) amewazo Real Madrid na euro 10.5 million kwa Lionel Messi alipwazo na Barcelona. Anzhi walifikia makubaliano na Internazionale kwa ada ya usajili dola 38.9 million tarehe 23 August 2011.
Anzhi inamilikiwa na Mwekezaji wa Ki-Russia Suleiman Kerimov, ambae ni tajiri wa 118 duniani akiwa na jumla ya utajiri uanokadiriwa dola 7.8 billion.

5. Wayne Rooney


2012  Mapato:€20.6 Million (pauni 17.2milioni)
2011  Mapato: €20.7 million
Utajiri Jumla: £45 Million or $72m – kufikia May 2012, habari kuhusu orodha ya Matajiri wa Uk kutoka the Sunday Times UK
Klabu Ya Sasa: Manchester United

Alipoteza mkataba na Coca Cola uliokua na thamani ya pauni 600,000-kwa-mwaka kwa tuhuma za uzinifu. Mchezaji huyo wa Manchester United striker alikua mchezaji wa Premier League anayeingiza pesa nyingi akijikusanyia euro 20.6m (pauni 17.2milioni) kwa mwaka. 
Hulipwa pauni 8milioni Old Trafford kwa msimu katika mkataba wake wa miaka mitano alioingia.

Baada ya kutemwa na Coca-Cola mwaka jana amebakiwa na Nike na Electronic Arts.

6. Sergio Aguero


2012  Mapato : €18.8 Million (£15.7m)
Utajiri Jumla: pauni 37 million (dola 59milioni)  – kufikia May 2011, habari kuhusu orodha ya Matajiri wa Uk kutoka the Sunday Times UK
Klabu Ya Sasa: Manchester City

Mshambuliaji wa ki-Argentina Sergio Aguero kwa sasa ndiye mshambuliaji wa kutumainiwa kwa klabu ya Premier League Manchester City na timu ys taifa ya Argentina.
Aguero alizivutia klabu kubwa Ulaya baada ya kuihama Independiente na kjiunga na klabu ya La Liga Atletico Madrid mwaka 2006.
Tarehe July 2011, mwanasoka huyo alijiunga na Manchester City kwa mkataba wa miaka mitano ulio na thamani ya ya pauni 35 million (€42.35 million), na kumfannya kua mwanasoka ghali zaidi aliyepata kutokea katika Historia ya klabu hiyo.

7. Yaya Touré


2012  Mapato: €17.6 Million (pauni 14.7milioni)
2011  Mapato: €13.8 Million
Utajiri Jumla: £12 Million ama $19m – kufikia May 2011, habari kuhusu orodha ya Matajiri wa Uk kutoka the Sunday Times UK
Klabu Ya Sasa: Manchester City

Kiungo wa klabu ya Premier League Manchester City na timu ya taifa Côte d’Ivoire. NI mdogo wa Kolo Touré wa Manchester City pia.
Touré alizawadiwa ufalme wa Mchezaji Bora wa Afrika kwa mwaka 2011. Touré aliihama Barcelona na kujiunga na Manchester City mwaka 2010 kwa ada ya pauni 24 million (€29 million) na kuingia mkataba wa miaka mitano unaokadiriwa kua pauni 55.6 million (€67.3 million).


8. Fernando Torres


2012  Mapato: €16.7 Million (pauni 13.9milioni)
2011  Mapato: €14 Million
Utajiri Jumla: £21 Million au$33.5m – kufikia May 2011, habari kuhusu orodha ya Matajiri wa Uk kutoka the Sunday Times UK
Klabu Ya Sasa: Chelsea

M-Spanish huyu ambaye hucheza kama mshambuliaji kwa Chelsea na timu ya taifa ya Spain, aliihama Atlético Madrid, akajiunga na Liverpool, na sasa yupo Chelsea, Torres amekua akitambulika kama mshambuliaji wa hali ya juu duniani.
Mwezi January 2011, Torres alijiunga na Chelsea kwa ada ambayo ni rekodi ya uhamisho Uingereza kwa pauni 50 million (€60.5 million) ndani ya mkataba wa miaka mitano na nusu, na kumfanya kua mchezaji ghali wa Ki-spanish kupata kutokea katika historia.

9. Ricardo Kaka


2012  Mapato: €15.5 million (£12.9m)
2011  Mapato: €19.3 Million
Utajiri Jumla: $100 Million – (makadirio)
Klabu Ya Sasa: Real Madrid

Kiungo mshambulizi wa Ki-brazilian ambaye kwa sasa anachezea Real Madrid na timu ya taifa ya Brazili. Kaka alitokea kwenye kava la gemu za soka EA Sports FIFA Soccer 11 na kuuza nakala 100 million. Wadhamini wakuu wa Kaka ni Adidas, Giorgio Armani na Guarana.

10. Philipp Lahm
2012  Mapato: €16.7 Million (pauni 11.9milioni)
2011  Mapato: €14 Million
Klabu Ya Sasa: Bayern Munich

Mchezaji wa Kimataifa wa Kijerumani ambaye ni nahodha wa timu yake ya taifa na klabu ya Bayern Munich.
Lahm anatambulika kama mmoja kati ya mabeki bora kabisa wa upande wa kushoto duniani.

JUMATANO NJEMAAAAAAAAAA!!!!!!

1 comment:

  1. If more of us valued food and cheer and song above hoarded gold, it would be a merrier world.
    - Personal loan with ABN AMRO Apply

    ReplyDelete