Sunday, September 9, 2012

Chelsea Kuendelea Na Chata La Samsung


Chelsea wamerefusha mkataba na wadhamini wao wa jezi Samsung mpaka mwisho wa msimu 2014-2015.

Mkataba una thamani ya pauni milioni 18 kwa mwaka.

Msemaji wa Chelsea alisema: 'Samsung wamerefusha mkataba nasi ambao utawafanya waendelee kua wadhamini wetu wakuu mpaka mwisho wa msimu May 2015. '

Kampuni hiyo ya vifaa vya umeme ya Korea ilisubiria mpaka Chelsea ilipochukua Ubingwa wa Ulaya ndipo wakaamua kurefusha mkataba.

Mapema mwaka huu, wapinzani wao kwenye ligi ya Uingereza Manchester United, walitangaza kuingia mkataba na Kiwanda cha Kusuka Mota na Injini ambapo moja ya brandi zao inayohusika na kuunda magari Chevrolet watakua wadhamini wa jezi zao kuanzia mwaka 2014 kwa ada ya pauni milioni 50 kwa kila msimu.

Hapa ndio utagundua kwa nini United ni klabu tajiri duniani: Chelsea pauni milioni 18 kwa mwaka wakiwa ni mabingwa wa Ulaya huku United watatia kibindoni pauni milioni 50 kwa mwaka huku hakuna kombe waliloshinda msimu uliomalizika.

JUMAPILI NJEMA!!!!!!!

No comments:

Post a Comment