Thursday, September 13, 2012

Juventus kutoa £10m kwa Winga wa Arsenal Walcott


Juventus wako tayari kuitest Arsenal kwa kutenga pauni milioni 10 kwa ajili ya kumnyakua Theo Walcott.

Winga huyo mwenye umri wa miaka 23 anaingia katika miezi 12 ya mwisho ya mkataba wake na Arsenal baada ya kugoma kusaini mkataba wa muda mrefu kwa mshahara wa pauni 75,000 kwa wiki.


Unsettled: Theo Walcott (left)


Alrsenal waliamua kutokumuuza Walcott kabla ya dirisha la usajili kufungwa baada ya kumwambia Wenger anataka kubakia Emirates.

Lakini mpaka sasa hakuna muafaka kwani Arsenal hawajakubali kumpa winga huyo kiasi anachokitaka (pauni 100,000-kwa-wiki).

Na mabingwa wa Italy Juventus wako tayari kumpa mshahara huo na zaidi iwapo Arsenal watakubali ofa yao.

Timu nyingine zinazomuwinda Walcott ni Liverpool, Manchester City na PSG. 

USIKU MWEMA!!!!!!!!!!

No comments:

Post a Comment