Tuesday, September 11, 2012

Man United wapanga Kumuuza Anderson


Kiungo wa Kibrazil anayeandamwa na majeraha kila msimu amekua Old Trafford kwa miaka mitano sasa na bado haonekani kua ameiva na hakuna dalili la hilo kutokea.
Wang on! Anderson clashes with Wang Shouting of Shanghai Shenhua during the pre-season friendly match. That's Wang Shouting.
Anderson akiwa katika mechi ya kujipima nguvu na Wang Shouting ya Shanghai Shenhua
Manchester United wanajitayarisha kumuuza kiungo Anderson katika dirisha dogo la  January ama majira ya joto yajayo.
M-brazili huyo haonekani kua amekwiva kama ilivyotarajiwa tokea alipojiunga na klabu hiyo mwaka 2007, na mazungumzo yalifanyika majira ya joto yaliyopita kuhusu kumuuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, huku Benfica na Tottenham walionesha nia ya kumtaka.
Anderson, ambaye alinunuliwa kwa pauni milioni 18, ana michezo 10 tu ya Premier League msimu uliopita na amekua anakumbwa na balaa la kua majeruhi tokea kujiunga kwake Old Trafford.
Sir Alex Ferguson, alipokua akichambua maisha ya soka ya Anderson huku akifananisha na bahati mbaya aliyoipata Michael Owen.
No chance saloon: Jonny Evans, Dimitar Berbatov, Michael Owen and Ji-Sung Park last autumn – only Evans remains...
Jonny Evans, Dimitar Berbatov, Michael Owen na Ji-Sung Park majira ya kipupwe yaliyopita – Evans tu ndiye aliyebaki...
Akimuongelea Anderson, Fergie alisema: “Hajafikia kiwango chake tulichotarajia, kitu kilicho wazi kwa yeyote kuona. 

“Ni mchezaji mzuri. Naomba asijepata bahati mbaya aliyoipata Michael Owen(kuumia umia) katika maisha yake ya soka.”

United hawana presha ya kumuuza Anderson katika dirisha dogo la January – mkataba wa Anderson utamalizikia mwaka 2015 – ila kuuzwa majira ya joto ndilo linaloonekana kuwepo...taarifa kutoka goal.com.
“Fergie amekua akisubiri bila mafanikio Anderson kufanya vema ila haionekani jambo hilo litatokea kwani hajawahi onekana katika kiwango bora tokea alipoumia goti mwaka 2010,” chanzo hicho kutoka United kiliiambia Goal.com. 
“Atawekwa sokoni kwa atakayetoa ofa nzuri, lakini bado ni mdogo na ana mkataba mrefu United hivyo hatuuzwa bei chee."
NAWATAKIA SIKU NJEMAAAAA!!!!!

No comments:

Post a Comment