Sunday, September 9, 2012

Frimpong Kurudi Mazoezini Ndani Ya Wiki MbiliKiungo wa Arsenal Emmanuel Frimpong mwenye miaka 20 anatarajia kuanza mazoezi ndani ya wiki mbili baada ya kua mkekani tokea February baada ya kupata majeraha akiwa Wolves kwa mkopo.

Hayo yamesemwa na yeye mwenyewe kupitia account yake ya twitter (twitter.com/Frimpong26AFC) alitwit: ' Nitarudi mazoezini tarehe 17 ya mwezi huu. Majeraha mara mbili ya kifundo cha mguu hayakuweza kunimaliza, ni muda mrefu wa miezi 7.'

Frimpong kurudi na nguvu mpya

Arsenal mpaka sasa bado hawajafungwa goli hata moja msimu huu na wamejikusanyia pointi tano katika michezo mitatu ya mwanzo waliyocheza.

Na kurudi kwa Frimpong kutawaongezea nguvu The Gunners katika nafasi ya kiungo hasa ikizingatiwa Alex Song kuihama timu hiyo na kujiunga na Barca hivi karibuni.

JUMAPILI NJEMA

No comments:

Post a Comment