Tuesday, September 11, 2012

Chelsea Ndio Klabu Bora Mwaka 2012


Chelsea imetajwa kua ndio klabu bora kwa mwaka huu 2012 na Chama Cha Klabu za Ulaya (European Club Association).

Mabingwa hao wa Ulaya walikabidhiwa taji lao hilo siku ya Jumatatu katika tamasha la tatu la ECA.

Euro joy: Chelsea's Frank Lampard with the Champions League trophy after beating Bayern Munich
Lampard akiwa na Kombe La Klabu Bingwa Ulaya baada ya kuifunga Bayern Munich
Chelsea walitunikiwa taji hilo baada ya kufanya vizuri katika msimu 2011-2012 katika ligi ya nyumbani na Ulaya. 

Msimu uliopita, The Blues walitia kikomo kusubiri kulinyanyua kombe la klabu bingwa ulaya na pia kufanikiwa kushinda kombe la FA, ingawa walimaliza wakiwa wa sita katika ligi ya Uingereza maarufu kama Barclays Premier League.

SIKU NJEMAAAAAA!!!!! 

No comments:

Post a Comment