Thursday, September 13, 2012

Mambo Yakienda Sawa Drogba Kutua Arsenal


Arsenal wako tayari kumpa ofa Didier Drogba ili ajiondoe Shanghai Shenhua ambapo mambo si mazuri.

Drogba mwenye umri wa miaka 34 amekumbana na balaa baada ya Bodi ya Wakurugenzi ya Shanghai Shenhua kutokuafikiana kuhusu matumizi ya timu hiyo hivyo kuuweka mkataba wake katika hatihati ya kuvunjwa miezi mitatu baada ya kuusaini kwa maafikiano ya malipo ya pauni 200,000 kwa wiki.

Uncertain future: Drogba and Nicolas Anelka have been caught up in a board room stand-off at Shanghai Shenhua

Arsenal wakiwa na pengo kubwa lililoachwa na van Persie aliyetimkia Man United, wamefanya mawasiliano na Wachina hao kuona kama kuna uwezekano wa kumrudisha Drogba London, The Sun limeripoti.

Liverpool na Real Madrid nao wanasubiria kama Drogba akionesha nia ya kuondoka, wafanye jitihada za kumpoka.

USIKU MWEMA!!!!!!!

No comments:

Post a Comment