Monday, July 2, 2012

BAADA YA EURO 2012, UINGEREZA NA KOMBE LA DUNIA 2014

          INAAMINIKA kwamba ligi ya Uingereza ndio bora na inayofuatiliwa zaidi duniani. Mafanikio ya kua na ligi kubwa hayajawa chachu ya kua na timu nzuri ya taifa. Sababu ni nyingi ila mimi nitajikita kwenye wachezaji wao walionao na kuakisi 2014.


Imekua ni kawaida Uingereza kufanya vibaya kwenye mashindano makubwa mfano dhahiri ni mashindano yaliyopita EURO 2012. Labda hatuwajui kwa undani wachezaji wao ndio maana hua tunataraji makubwa, hapa nitachambua kwa kina kila mchezaji na umri watakaokua nao kufikia WORLD CUP BRAZIL kwa kuzingatia mchango wao  mwaka 2014 

Vichwa chini: kwa mara nyingine Uingereza wameshindwa kuthibitisha wao ni kati ya miamba ya soka duniani. 


Kufikia mashindano ya World Cup 2014 nchini Brazil,  Steven Gerrard atakua na miaka 34, Scott Parker atakaribia 34, John Terry  na Ashley Cole 33 na miezi sita. Wengine ambao ni tegemeo kama Frank Lampard atakua 36 na Gareth Barry 33, kama ilivyo kwa Peter Crouch, wakati Rio Ferdinand ambaye anaweza itwa tena baada ya kujinadi hajafunga milango kuchezea timu ya taifa lake basi kufikia 2014 ye atakua na miaka 35.



Wachezaji nane niliowaaja hapo juu Ashley Cole ndiye pekee anayeonekana kua na uhakika ila bahati hiyo haionekani kuwepo kwa captain wake John Terry ingawa tofauti ya umri wao ni siku 13 tu. 


Kwenye ukuta wa Uingereza timu nyingi zilionekana kumkusudia John Terry kwa mipira ya juu na ya kufukuzia. Italy walirusha mipira moja kwa moja kwake, kama walivyofanya Wajerumani na athari zilionekana ila si kwa kiwango kikubwa. Ikizingatiwa Hudgson ameshasema  anataka ukuta imara basi inaonekana kutakua na mabadiliko kwenye ngome hiyo.

Goli si Goli: Terry amekua mtu wa bahati na maamuzi mengi huangukia kwake, mwisho wa bahati ni mwisho wa kuiwakilisha uingereza.



Baada Garry Cahill kuumia kabla ya EURO 2012, Jeleon Lescott aliitwaa kitu kinachoonesha hayuko mbali na mipango ya Hudgson. Na kama hilo ndilo na akaendelea kumuamini basi atakua beki wa kati mkubwa Brazil kwenda miaka 31 kama Terry na Rio wakiachwa nyumbani.


 Kwa maana nyingine Cahill ndiye anayeonekana atakua mwenza wake ila waingereza wengi wanaombea Phil Jones ambaye atakua na miaka 22 na Smalling (24) kuendelea kujituma zaidi kuchukua nafasi hizo.





Kwa sasa Jones na Smallin bado hawajapata uzoefu stahili kutengemewa kama mabeki wa kati, mara kwa mara wamekua wakitumiwa kama mabeki wa pembeni pindi wenye nafasi wakikosekana. Hayo wanaweza pia semwa kwa Micah Richards.
Richards ni mbichi ila anaonekana anaweza kufanya vema kwenye nafasi zote mbili akipata michezo ya kutosha. 


Baada ya Cahill kuumia hakujitendea haki kwani  tayari alikua ameshatimkia visiwa vya Caribbean kwa mapumziko. Kitu kilichomlazimu Hodgson kumuita kinda Martin Kelly wa Liverpool. 


Mchezaji huyo wa Manchester  City atakua na miaka 26 majira ya joto 2014, akiwa anajilaumu kwenda mapumziko mapema kwa hasira ya kutemwa timu ya taifa, sasa itabidi atilie maanani kupata nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha Manchester City ili ajihakikishie kutokwenda mapumziko mapema wakati wenzake wakijiandaa kwenda Brazil.



Inaonekana ni rahisi kwa Jones ama Smalling kumuondoa kikosini Terry kuliko wao kumuondoa  Glen Johnson pembeni. Beki huyo wa kulia wa Liverpool, atakua na miaka 29 majira ya joto 2014, kwa kipindi chote cha uchezaji wake timu ya taifa hajawahi kua kipenzi cha mashabiki wa Uingereza, labda Kyle Walker wa Spurs (24 mwaka 2014) anaweza kumpoka namba beki ya kulia hatokua na cha ziada zaidi ya kukaba.


Kyle Walker: Beki mkimbizaji anayenyemelea nafasi ya Glen Johnson.


Fomesheni ya Uingereza 4-4-2 kuibadili kua ya kisasa inahitaji mabeki wa pembeni kurandaranda zaidi kwenye nusu ya wapinzani kuliko sasa kwa mfumo ya kujilinda zaidi. Kama Hudgson akimua kujilinda kwa kushambilia badala ya sasa ya kujilinda kwa kukaba basi Kyle Walker kwa upande wa kulia anaonekana kua chaguo namba  moja. 




Beki wa kushoto,ina kina Kieran Gibbs wa Arsenal ukiachilia mbali majeruhi ya mara kwa mara anaweza kukaba kwa kushambulia, Leighton Baines ni mbora kwa shughuli hii na ndiye hasa anayeonekana kusuburi nafasi yake upande wa kushoto. Cole akiteleza, Hodgson hatosita kumpa nafasi Baines kwa ubora  wake wakupiga krosi nzuri na kwa haraka ndani ya kumi na nane akiwa kwenye spidi kubwa.


Baines ataendelea kumpa presha Cole kwa nafasi ya beki wa kushoto.




Steven Gerrald ametangaza hivi karibuni hana nia ya kuachia ngazi, atakua na miaka 34 May 2014, ikiwa msingi wa mchezo wake ni kuzuia na kuanzisha mashambilizi kutokea pande zote za kiwanja kwa umri miaka 34 2014 uwezo wake hutakua huu tuliouzoea. 




Kwenye Euro 2012 amekua na mchezo mzuri na ndiye Muingereza pekee kuchaguliwa kwenye timu ya EURO 2012. Takwimu zinaonesha anaongoza kufanya tacling (kunyan'ganya mipira miguuni mwa mpinzani) zisizo na madhambi. Kama miguu yake haitomuangusha kwa umri na akawa anacheza salama mbele ya mabeki wake kuliko kucheza mbele ya mabeki wa timu pinzani basi atakua na cha kusaidia huko Brazil.



Ilikua vigumu kumfikiria Scott Parker miaka miwili iliyopita, Tatizo lake si mchezaji wa dakika 90. kwa nguvu nyingi atumiazo na jitihada zake uwanjani kufikia dakika ya 70 ye hua hoi. Tofauti na hayo pasi salama zifikazo kwenye mguu wa aliyemdhamiria na kuvuia mashuti kwa kukinga mwili wake ndio ngao yake kuu.




 Kama ilivyo Barry na Lampard, mpaka kufikia 2014 anaweza kua kasahaulika kabisa, nikikukumbusha waliochaguliwa kwenda South Africa kina Matthew Upson, Emile Heskey na Shaun Wright-Phillips ambao kwa sasa hata kufikiriwa hawafikiriwi chochote kinaweza kutokea.



Kama kuna dua Uingereza wanayoomba basi ni kumuona Jack Wilshere akirudi dimbani,  kipaji cha ubunifu, na maamuzi makubwa licha ya umri wake mdogo vitaongeza ufundi katikati ya uwanja. 


Tom Cleverley, Jack Rodwell, Josh McEeachran na Jordan Henderson, aliyeitwa EURO 2012 kutokea orodha ya wachezaji wa akiba kukamilisha watu 23 baada ya Michael Carrick kukataa kuwemo kwenye orodha hiyo. Iwapo asingekataa basi ye ndiye ambaye angeitwa. Carrick atakua na miaka 34 kufikia 2014 kwa umri huo na kutokuzingatiwa ni dhahiri hana chake.



Mawinga: kwa muundo wa Kiingereza ambao ni kujilinda zaidi, mawinga chaguo la kwanza Ashley Young na James Milner, ambao kwenye mashindano ya Euro 2012 hawakufanya lolote la maana kama mawinga, watakua na miaka 28 mwaka 2014. Kama muundo huo utabadilika na kua kujilinda kwa kushambulia basi Theo Walcott na Alex Oxlade-Chamberlain watakua waanzaji bila kikwazo, kuna wengine kama kina Aaron Lennon, Adam Johnson na kama atarudi kwenye fomu – Gabriel Agbonlahor.





Walcott na Oxlade-Chamberlain wote watapigania kuanza zaidi ya kutumika kama wabadilisha matokeo.



Kuna Danny Sturridge, ingawa ni mchezaji asiyependa kurudi nyuma kukaba wala kucheza pembeni kama winga: anasisitiza ye ni mshambuliaji si winga. Ushambilizi wapo kina Wayne Rooney  ambaye atakua 28. 


Andy Carroll atakua na 25 na Danny Welbeck (23) itabidi Sturridge afanye vema kumuondoa mmoja wapo, licha ya kua atakua na umri mdogo Andy Carrol anatakiwa kuthibithisha thamani yake nili sturridge aendelee kusubiri. 

Si ajabu  tukashuhudia mwanzo wa vizazi vipya hasa wachezaji wa Uingereza chini ya miaka 21 wanaofaya vizuri kwa sasa (England U21)  kina Steven Caulker wa Tottenham, Evertonian Ross Barkley na mcheza wa Palace Wilfried Zaha.




Kufikia 2014 Jermain Defoe ataakua 31, Darren Bent 30, vipi wataendelea kupuuziwa na makocha wa Uingereza ingawa rekodi zao kwenye vilabu na timu ya taifa zinavutia ama ndio utakua muda wa kuthibitishia ulimwengu kua walikua wanaachwa ki makosa? 




Kwa maajabu ya soka pia kuna uwezekano akaibuka mtoto ambaye hata sijamuongelea hapa kuishika dunia kwa mabao yatakayowapaisha Uingereza. 





 Uchaguzi Wangu Wachezaji 23 kwa 2014 Brazil 



MAKIPA: Hart, Ruddy, Carson


WALINZI: G.Johnson, Walker, Cahill, Lescott, Jones, Smalling, Cole, Baines


VIUNGO: Gerrard, Wilshere, Cleverley, Rodwell, Oxlade-Chamberlain, Walcott, Young, Adam                             Johnson

WASHAMBULIAJI: Rooney, Welbeck, Carroll, Sturridge





Nini wazo wazo lako, changia hapo chini .....................................................................!!!!!!!

No comments:

Post a Comment