Rusia usajili wao ulifungwa rasmi jana saa sita usiku kwa masaa ya Ulaya, hivyo kulikua bado na uwezekano wa Nani kuondoka Man U ingawa dirisha la Usajili lilikua limeshafungwa Uingereza na sehemu nyingi za Ulaya.
Nani ambaye alikua ameruhusiwa kuondoka Manchester United, hataondoka tena kwa sababu ya mshahara mkubwa aliokuwa anataka awe analipwa na klabu hiyo.
Nani ambaye pia bado hajakubali mshahara mpya aliotengewa na Mashetani Wekundu kama ataamua kubaki, yuko njia panda Old Trafford kwani si tu amegomewa kukubaliwa kua analipwa pauni 130,000 kwa wiki bali hata uhakika wa nafasi kiwanjani hana.
Nani na GF wake wakiwa katika hafla kuchangia Unicef iliyoandaliwa na United |
Watu wa karibu yake wanasema kwamba Nani anajiona hathaminiwi United kama wachezai wengine.
Aliondolewa kikosini baada ya United kupata kipigo katika mechi ya ufunguzi dhidi ya Everton na tokea wakati huo hana uhakika wa namba.
Kagawa anapata nafasi zaidi kulika Nani |
ALHAMISI NJEMA!!!!!!!!!!!!
No comments:
Post a Comment